Habari za Punde

Tuwatathmini mawaziri, wakurugenzi baada ya mwaka mmoja wa fedha


Na Haji Nassor, Pemba
MWEZI uliopita, wajumbe wa baraza la Wawakilishi Zanzibar, kama chombo huru, walimaliza kazi za kuzijadili na kuzipitisha bajeti za wizara 13 za SMZ, ili mawaziri hao wakaanze kazi.
Hatua hiyo ni moja tu, lakini ya na pili ni kuanza utekelezaji wa bajeti zenyewe, na hasa kwa vile mawaziri walionekana kuwa na hamu ya kazi wakati wakijitetea ndani ya baraza hilo.
Wapo wanaoendelea kuguna, kucheka, kupata wasiwasi, ilioambatana na hofu, kuwa mawaziri hao,  eti hawana jipya kwenye kazi zao, licha ya kuonekana kumwagika machozi wakati wakiwa juu ya viriri vya kupitisha bajeti.
Ndio maana nasema kuwa, ni vyema tuwatathimini waziri, wakurugenzi baada ya mwaka mmoja wa fedha, badala ya kuanza kusema ndio hayo hayo ya kila siku.
Kwanini muwe na haraka kwa mawaziri, wakurugenzi na makatibu wakuu wateule, juu ya kutekeleza ahadi walizoziweka iwe kwa wafanyakazi au jamii husika.
Sio busara utendaji wa kazi kwa kiongozi aliepita kwa kushindwa kutekeleza ahadi zake, na kila ajae kuanza kuguna au kumtafsiri kama aliepita, wakati huu bado hata bajeti walizozipitisha hawajaanza kuzitumia.
Naam…..wapo watendaji wamekuwa wakizungumza vibaya kwa eti wateule wa hivi karibuni hawatarajii kuwa na jipya, ingawa wanasema hayo wakiangalia walikotoka, lakini yote kwa yote bado mapema.
Hebu tusubirini, tukaeni kimnya, tuwape nafasi walau mwaka huu wa na bajeti 2016/17 umalizike, na kisha tuone zile ndaro na majigambo yao wakati wakiwa ndani ya mjengo.
Sio wapo walioahidi kwamba wanahamu ya kazi kama Mhe: Rais alivyowataka, sasa tuwape mwanya kwanza na wala tusianze kuwabeza na kudharau, wakati huu wakiwa hawajapata vitendea kazi.
Kwani sio kila wizara imeomba bajeti yake na kila waziri au mkuregenzi amejinasibu kuwa yeye ni mbunifu kwenye kazi zake, sasa iweje tuanze kuwapa mgongo mapema kuwa hawana uwezo.
Kwani mwaka huu wa fedha wala hauko mbali, na wameshaahidi kwamba watahakikisha haki za wafanyakazi, wataziangalia kwa jicho jengine, sasa iweje wajitokeze wachache waanze kupata hofu kwa wateule wetu.
Kama tunamuani kiutendaji rasi wetu mpendwa dk Ali Mohamed Shein, basi wala tusifanye haraka kuwahumu wateule wake wala kujihitimu kuwa hakuna jipya, hebu tusibirni kwanza.
Walishasema wazee kuwa haraka haraka haina baraka, wengine wakaibuka kuwa chanda chema hivishwa pete, sasa lazima na sisi tuwape muda wateule.
Yote kwa yote lazima tuwe wastahamilivu kwa wateule watu na kuwasubiri walau mwaka mmoja wa fedha wa umalizike huku tukiwapa ushirikiano wa karibu.
Lakini nanyi watuele lazima muandamane na kasi ya kweli ya kiongozi wetu wa nchi, ambayo ameshasema lazima tuachane na kufanya kazi kwa mazoea.
Mimi naamini kila jambo linawezekana kutendeka kwa uri iwapo kila mmoja atafanya kazi zake kwa kufuata sheria na taratibu ilizopo huku rushwa na muhali ukiwekwa pembeni.

                      hajinassor1987@gmail.com 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.