Habari za Punde

Ufunguzi wa Mashindano ya Airtel Rising Stars Wafanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar.

Baadhi ya Timu mbalimbali za Wanawake ambazo zinashiriki katika mashindano ya Airtel Rising Stars zikiwasili katika Ufunguzi wa mashindano hayo uliofanyika katika Kiwanja cha Amani Zanzibar.
Meneja wa Airtel Zanzibar Muhidini Mikidadi akitoa maelezo kuhusu mashindano ya Airtel Rising Stars kwa timu za  wanawake yaliofunguliwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utalii Utamaduni na Michezo Zanzibar Hassan Abdalla Mitawi katika Uwanja wa Aman.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utalii Utamaduni na Michezo Hassan Abdalla Mitawi akitoa hotuba ya Ufunguzi katika Mashindano ya Airtel Rising Stars kwa timu za Wanawake katika Uwanja wa Amani Zanzibar. 
Baadhi ya Waalikwa waliohudhuria katika Ufunguzi wa mashindano ya Airtel Rising Stars kwa timu za Wanawake katika Uwanja wa Amani Zanzibar.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utalii Utamaduni na Michezo Hassan Abdalla Mitawi akikagua Timu mbalimbali zinazoshiriki katika Mashindano ya Airtel Rising Stars Uwanja wa Amani Zanzibar.
Mchezaji wa Timu ya Jumbi Wilaya ya Kati (Women Fiter)Monica Josef akijaribu kumzuia mchezaji wa Timu ya Bungi katika mashindano ya Airtel Rising Stars baada ya kufunguliwa leo Uwanja wa Amani Zanzibar.
(Picha na Yussuf Simai Maelezo)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.