Habari za Punde

Ujumbe kutoka Manispaliti ya Sundsvall Sweden Watembelea Jengo la Baraza la Wawakilishi Zanzibar.

Kaimu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Mgeni akitoa maelezo kuhusu shughuli za Baraza lake kwa ujumbe wa watu watatu kutoka Manispaliti ya Sundsvall.  Katika picha anaonekana ndugu Bjorh Sweden na bi.  Christin Strömberg.  Aidha katika mazugumzo hayo naibu spika ameutaka ujumbe huo kuendelea kuimarisha uhusiano wao na wadi ya Makunduchi katika sekta ya elimu ili kuongeza ufaulu wa wanafunzi hapa nchini 
Ujumbe wa watu watatu kutoka Manispaliti ya Sundsvall ukiwa katika afisi ya Hansard ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakipatiwa maelezo utendaji wa kila siku wa sehemu hiyo. 

Ujumbe kutoka Manispaliti ya Sundsvall Nchini Sweden ukiwa katika ziara yake Zanzibar imepata nafasi kutembelea Baraza la Wawakilishi Zanzibar na kufanya mazugumzo na Naibu Spika Mhe. Mgeni. wakiwa Katika picha ya pamoja kutoka kushoto Mratibu wa Uhusiano kati ya Wadi ya Makunduchi na Manispaliti ya Sundsvall Ndugu Mohamed Muombwa, Trevor Fisher, Mhe. Abdulla A. Kombo Mwakilishi wa Jimbo la Mwanakwerekwe,Kaimu Spika Mhe.Mgeni Hassan, Christin Strömberg.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.