Habari za Punde

Afisi ya Baraza la Wawakilishi Yawaaga Wafanya Kazi Wake Wastaafu kwa Utumishi Uliotukuka..

Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zuberi Ali Maulid na Spika Mstaaf Mhe Pandu Ameir Kificho wakiwa na Maofisa wa Baraza wakisimanma kwa dakika moja kuwaombea Wafanyakazi wa Baraza waliofariki dunia wakati wa hafla ya kuwaaga Wafanyakazi hafla hiyo imefanyika katika ukumbi mdogo wa Baraza Chukwani Zanzibar.
Wafanyakazi wastaaf wakiwa wamesimama kuwaombea wafanyakazi waliofariki kabla ya kuaza kwa hafla hiyo. 
Wafanyakazi wa Baraza la Wawakilishi wakiwa wamesimama kwa dakika moja kuwaombea dua Wafanyakazi wa Baraza waliofariki dunia wakiwa watumishi wa Baraza. 
Mkuu wa Utawala na Rasilimali Watu  Amour Mohammed akitowa wasifu wa Wafanyakazi Wastaaf wa Baraza wakati wa kuwaaga.  hafla hiyo imefanyika katika ukumbi mdogo wa baraza chukwani Zanzibar.

Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Zuberi Ali Maulid na Spika Mstaaf Mhe OPandu Ameir Kificho wakifurahia jambo wakati wa kutajwa kwa Wasifu wa Wafanyakazi Wastaaf wa Baraza katika hafla ya kuwatunikia zawadi kwa Utumishi wao uliotukuka. 
Wafanyakati wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakiwa katika ukumbi wa hafla ya kuwaaga wafanyakazi wastaaf wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar. 
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zuberi Ali Maulid akimkabidhi zawadi ya Seti ya TV Mfanyakazi Mstaaf wa Baraza Bi. Zulfa Haji Wadi.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zuberi Ali Maulid akimkabidhi zawadi ya Seti ya TV  na saa ya ukutani Mfanyakazi Mstaaf wa Baraza Bi.Moza Abdallah Jabir. 
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zuberi Ali Maulid akimkabidhi zawadi ya Seti ya TV na Saa ya ukutani Mfanyakazi Mstaaf wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Haji Othman,. 
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zuberi Ali Maulid akimkabidhi zawadi ya Seti ya TV na Saa za ukutani Mfanyakazi Mstaaf wa Baraza Mzee Muhidin  Haji Makame . 
Spika Mstaaf wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Pandu Ameir Kificho akitowa nasaha zake kwa Wafanyakazi wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakati wa hafla hiyo ya kuwaaga Wafanyakazi Wastaaf Tisa wa Baraza.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zuberi Ali Maulid akizungumza na Wafanyakazi wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakati wa hafla ya kuwaaga wastaaf hao kwa utumishi wao uliotukuka jumla ya Wafanyakazi tisa wastaaf wameagwa katika hafla hiyo.Mfanyakazi Mstaaf wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Bi Moza Abdallah Jabir,akitowa shukrani kwa niaba ya wezake wakati wa hafla hiyo ya kuwaaga iliofanyika katika ukumbi mdogo wa mikutano wa Baraza Chukwani Zanzibar.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Zuberi Ali Maulid na Spika Mstaaf Mhe Pandu Ameir Kificho wakiwa katika picha ya pamoja na Wastaaf na Wafanyakazi wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar. baada ya kumalizika kwa hafla hiyo iliofanyika katika ukumbi mdogo wa baraza chukwani Zanzibar. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.