Habari za Punde

Balozi Seif akutana na Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Cuba

 Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Cuba Bwana Salvador Antonio Valdes Mesa wa Tatu upande wa Kushoto na ujumbe wake akizungumza na mwenyeji wake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wa kwanza kulia ofisini kwa Balozi Seif Vuga Mjini Zanzibar.
 Balozi Seif akimuonyesha mgeni wake Bwana Salvador baadhi ya vitu vya utamaduni kama kanga pamoja na vyakula vya viungo alivyomuandalia kama zawadi ya uwepo wake Visiwani Zanzibar.
 Balozi Seif akimkabidhi zawadi ya Kasha Makamu wa Rais wa Cuba Bwana Salvador likisheheni vitu vya utamaduni na vyakula vya viungo mara baada ya kumaliza mazungumzo yao.

 Balozi Seif wa Nne kutoka Kulia na Mgeni wake Bwana Salvador wanne kutoka kushoto wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine walioshiriki kwenye mazungumzo yao ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kulia akimuaga mgeni wake Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Cuba Bwana Salvador Antonio Valdes Mesa mara baada ya mazungumzo yao.

Picha na – OMPR – ZNZ.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.