Habari za Punde

Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania Jasem Alnajim Atembelea Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar.

Balozi wa Kuweit nchini Tanzania Jasem Alnajim akimkabidhi Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Juma Malik  Akili msaada wa moja ya  mashine  tatu za kupimia Presha alipotembelea Hospitali Kuu ya Mnazi mmoja mjini Zanzibar.
Balozi wa Kuweit nchini Tanzania Jasem Alnajim akiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Juma Malik Akili wakiwapa zawadi akinamama waliojifungua katika wodi ya wazazi ya Hospitali kuu ya Mnazi mmoja.
Balozi wa Kuweit nchini Tanzania Jasem Alnajim akimbeba mtoto mchanga alipotembelea wodi ya wazazi ya hospitali  kuu ya Mnazi mmoja Mjini Zanzibar.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali kuu ya Mnazi mmoja Dkt. Ali Salum Ali akimuongoza Balozi wa Kuweit nchini Tanzania Jasem Alnajim alipotembelea majengo mapya ya Hospitali hiyo yaliyofunguliwa hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.