Habari za Punde

Rais Magufuli ampokea Rais wa Zambia leo

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Dkt John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake  Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Chagwa Lungu wakisimama kwa ajili ya nyimbo za Taifa na mizinga 11 mara  baada ya kiongozi huyo kuwasili katika uwanja wa  ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam jioni ya leo Novemba 27, 2016

 Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Chagwa Lungu akikagua gwaride rasmi i mara tu baada ya kupokewa na mwenyeji wake Rais Dkt John Magufuli katika uwanja wa  ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam jioni ya leo Novemba 27, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Dkt John Pombe Magufuli akimtambulisha Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Chagwa Lungu kwa Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe kassim Majaliwa baada ya kuwasili katika uwanja wa  ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam jioni ya leo Novemba 27, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Chagwa Lungu akisalimiana na mabalozi wanaowakilisha nchi mbalimbali za Afrika nchini mara tu baada ya kupokewa na mwenyeji wake Rais Dkt John Magufuli katika uwanja wa  ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam jioni ya leo Novemba 27, 2016

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.