Benjamin Sawe-MAELEZO
Katika kipindi cha mwaka mmoja wa
uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano kumefanyika jitahada kubwa za kuhakikisha
inafufua mashirika yalifikia hali mbaya
na kushindwa kutoa huduma ili hatimaye yaanze upya kutoa mchango wa ujenzi wa uchumi nchi.
Mojawapo wa Mashirika hayo ni pamoja
na Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL) ambapo kabla ya Rais Magufuli kuingia
madarakani lilikuwa na Ndege mmoja tu.
Hatua hiyo ya Rais Magufuli kuamua kununua
Ndege mbili aina ya Bombadier Q400 zimesaidia kuimarisha Kampuni hiyo na kurejesha nembo ya Twiga
iliyoanza kupotea.
Licha ya juhudi hizo na kazi mkubwa
aliyoifanya Rais Magufuli ya kutimiza ahadi yake ya kuanza kuijenga upya
Kampuni hiyo, wapo baadhi ya wananchi wachache ambavyo wamewakuwa hawana
shukurani na kuanza kubeza jitihada hizo.
Ni vema wakumbe ule usemi unaotumiwa
na baadhi ya watu kuwa “ Hata mbuyu ulianza kama mchicha” .Kauli
hii inadhihirisha kuwa kila jambo uwa na mwanzo wake kwani tokana na dhihaka za
baadhi ya watu ambao wamekuwa wakibeza juhudi za Mhe. Rais Magufuli.
Ununuzi wa Ndege hizo umesaidia kumeimarisha
huduma za usafiri wa anga na kuongeza ushindani katika utoaji wa huduma za anga
hapa nchini kati yake na kampuni binafsi za ndege zinazotoa huduma hiyo kwa
sasa
Azma hiyo ya Serikali ya kununua ndege
mpya imetimiza ahadi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John Pombe
Magufuli wa kulifufua tena Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) na kulipatia mtaji
ili lianze upya kutoa huduma hiyo kwa Watanzania.
Akizindua ndege hizo Rais Magufuli
alisema kuwa ,ndege hizo zina sifa ya matumizi madogo ya mafuta na ni suluhisho
la kupanda kwa bei ya usafiri wa anga nchini na pia zitasaidia kukuza sekta ya
utalii nchini.
“Ndege hizi zinatumia wastani wa
mafuta ya shilingi milioni moja kutoka hapa hadi Songea, wakati ndege za Jet
zinatumia mafuta ya shilingi milioni 28.1 kwa safari kama hiyo,” anasema
Mheshimiwa Rais.
Ukitaka
kujenga nchi yenye uchumi wa kisasa huwezi kujenga bila kuwa na ndege na
ukitaka watalii lazima uwe na ndege.
“Tunataka watalii wanaokuja nchini
kuja moja kwa moja bila kushuka nchi nyingine ili kuongeza mapato yetu na
kukuza utalii duniani na kuwa na ndege nyingi zaidi kama nchi nyingine” anasema Rais
Magufuli.
Mbali na kuleta ndege hizo, yapo mambo
mengi makubwa ambayo Rais Magufuli ameanza kuyatekeleza, aliyoahidi wakati wa
kampeni za uchaguzi mkuu mwaka jana, hatua ambayo imewavutia watu wengi ndani
na nje ya nchi.
Aidha
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa leo alizindua awamu ya kwanza ya upanuzi wa Uwanja
wa Ndege wa Dodoma ili uweze kupokea ndege kubwa za mizigo, abiria na viongozi
wa kitaifa na kimataifa.
Uzinduzi
huo ni miongoni mwa maandalizi ya kutimiza azma ya kuufanya mkoa wa Dodoma kuwa
Makao Makuu ya Tanzania. Ujenzi huo umegharimu Sh bilioni 11.5 ambazo ni fedha
za ndani na utatoa fursa kwa mashirika ya ndege kuanza huduma Dodoma, ikiwemo
ndege ambazo zimenunuliwa na serikali.
Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana anasema, uzinduzi huo hautaathiri mchakato
wa kujenga Uwanja wa Ndege wa Kimataifa eneo la Msalato.
“Mchakato wa ujenzi wa uwanja wa ndege Msalato
uko pale pale,” anasema Rugimbana na kuongeza kuwa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano imeamua kufanya upanuzi wa uwanja huo ili ndege kubwa zitue
mkoani humo.
‘’Wizara
ya Ujenzi imeamua kufanya upanuzi wa uwanja wetu wa ndege wa Dodoma ili ndege
kubwa ziweze kutua na sisi tunamshukuru Rais kwa kutupa uwanja huo kwani
utazidi kufungua fursa katika mkoa wetu,” anaeleza Rugimbana.
Rugimbana
anasema sababu ya kupanuliwa uwanja huo ni nia ya dhati ya Rais Magufuli ya
serikali yake kuhamia Dodoma.
Alisema
baada ya uzinduzi huo wa awamu ya kwanza, awamu ya pili itafanyika kwa haraka
ili uwanja huo uweze kukamilika kama ilivyopangwa.
Upanuzi
wa uwanja wa ndege wa Dodoma unahusisha njia ya kuruka na kutua kwa ndege,
yenye urefu wa kilometa 2.5 na mita 500 za taa za kuongozea ndege na usalama wa
kuruka kwa ndege.
Nae,
ofisa mwandamizi wa uwanja huo, Emmanuel Kisumo anasema kwa sasa uwanja huo
umepata uhai mpya baada ya mradi huo kukamilika.
Shirika letu la ndege lilikuwa na hali
mbaya kutokana na kushindwa kujiendesha kutokana na gharama kubwa za uendeshaji
na abiria wachache, wanaotumia usafiri wa anga na kwa hili Mheshimiwa Rais
anastahili pongezi kwa kulifufua Shirika hili.
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake
mpeni, Hongera Mheshimiwa Rais kwa mafanikio ya kutununulia ndege mbili mpya
kwa kipindi kifupi sana cha mwaka mmoja.
No comments:
Post a Comment