Habari za Punde

UVCCM waanza kutimiza ndoto zao kwa vitendo

 Kaimu katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka (MNEC)aki zindua ofisi ya Umoja wa Vijana Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.
 Kaimu katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka (MNEC)aki Fungua ofisi ya Umoja wa Vijana Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara
 Muonekano wa Ofisi mpya ya Umoja Wa Vijana Wilayani Simanjiro Ilio zinduliwa Na Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka (MNEC)
 Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka akizungumza na Wana chama na Viongozi Mbali mbali mara baada ya kupokelewa Wilayani Simanjiro

Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka akizungumza na Wana chama na Viongozi Mbali mbali mara baada ya kupokelewa Wilayani Simanjiro




SHAKA ahimiza utendaji wa pamoja na ubunifu
Na Mwandishi Wetu, Simanjiro

Kaimu Katibu Mkuu  wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka amesema mtendaji au kiongozi wa jumuya hiyo  atakayeshindwa kuwa mbunifu, kuibua mambo  au kutofanya kazi kwa kutofuata kanuni ikiwemo na kutoyaelewa malengo ya Serikali ya Chama Cha Mapinduzi atapungukiwa na sifa ya kuendelea kushika dhamana muhimu.

Amesema ni jukumu la kila mtendaji au kiongozi katika ngazi yake kufanya kazi kwa ufanisi  pamoja na kuonyesha kipaji na uwezo binafsi wa kubuni masuala  ya msingi yatakayoweza kuipa hadhi na heshima jumuiya hiyo mbele ya CCM na jamii.

Shaka alitoa matamshi hayo leo huku akisistiza kuwa UVCCM wanakoelekea hivi sasa haitamuonea haya wala soni mtendaji au kiongozi yeyote ambaye amepewa dhamana na hataonyesha uwezo wa kuisaidia jumuiya hiyo kimaendeleo. Alieleza hayo muda mfupi baada ya kuzindua jengo jipya la kisasa  la ofisi ya UVCCM la wilaya ya  lililojengwa kwa gharama ya zaidi ya shillingi  10,400, 020 fedha taslim michango ya vifaa kutoka kwa wadau na nguvu kazi ya vijana wa Simanjiro Mkoani Manyara.

Alisema kitendo cha kijana yeyote kukabidhiwa jukumu ndani  ya  jumuiya ya vijana ya chama tawala, kwanza anahitaji kujivunia hadhi aliopewa   pia aone  fahari katika maisha yake kwa kubahatika kuitumikia jumuiya ya chama kinachoongoza dola .

"Ikiwa umepata dhamana ya kukabidhiwa majukumu ya kiutendaji au kiungozi  shirikisha pia shirikiana na wenzako , washirikishe katika utekelezaji wa majukumu ya kiutendaji, kataa kufanya maamuzi kwa hiari au  utashi wako, utendaji wa pamoja una faida kuliko maamuzi binafsi "alieleza Shaka.

Kaimu huyo Katibu Mkuu aliusifu uongozi wa UVCCM  Mkoa wa Manyara hususan watendaji na wajumbe wa kamati  utekelezaji na Baraza kuu katika wilayani ya Simanjiro kwa kuonyesha kwao umoja ulioleta mafanikio kwa kubuni,  kujenga na kumaliza  jengo jipya la UVCCM la kisasa 

"Kaa katika nafasi yako ya utendaji au uongozi  ili siku moja ukiondoka wenzako wakukumbuke, historia ikuandike na kukuenzi , huwezi kupendwa na wote ila asilimia kubwa ikutaje kwa mema kuliko mabaya, tunataka ubunifu badala ya majungu na na kugawa watu"Alisema

Aidha Shakaisema wapo baadhi ya wana jumuiya wanaofikiri ili awe  kiongozi analazima kuwa  uhodari wa kuwagawa watu, kupika majungu, kueneza maneno yanayoleta mgawanyiko huku akiwa hana uwezo wa kutimiza majukumu aliokabidhiwa katika ngazi yake.

Alisema aina ya viongozi hao hawatapata nafasi tena ndani ya UVCCM badala yake siku zote watakuwa wakiangalia kuchuja na kupembua  nani ana dhamira njema, nia thabit  , uwezo na uaminifu wa kuitumikia jumuiya hiyo si vinginevyo .

"Mara nyingi kila mtoto anayebebwa mbelekoni hukitazama kichogo cha mama yake, kiuongozi au mtendaji wa UVCCM naye aitazame spidi ya Serikali ya CCM kisha ajipime kama anatosha au la, kama hawezi aseme ili apumzishwe kuliko kuboronga "alisisitiza shaka .

Mapema Mwenyekiti wa  UVCCM Wilaya ya Simanjiro Kiria Ole Laizer alisema ni wajibu wa kila mtendaji wa jumuiya hiyo kuelewa na kutambua mipaka na jukumu lake, kusimamia na kutekekza kwa maarifa na ufanisi.

Ole Laizer aisema jumuiya ya UVCCM ndiyo  moyo na shamba bora  linalotegemewa kutoa mavuno yenye tija kwa uongozi bora ambao utashika hatamu za utawala na kuendsha medani za madaraka kwa weledi, ujuzi, nidhu na maarifa.

Katibu Mkuu shaka amechangia millioni moja kuchangia ununuzi wa thamani za ofisi na computer seti 1

Wilaya ya Simanjiro imekuwa wilaya ya kwanza kutekeleza agizo hilo lilitolewa mwezi mei 2016 ambapo Unchini nzima wameagizwa kujenga majengo ya kisasa ya ofisi nyumba za watumishi na kuanzisha miradi ya vitega uchumi ambapo hadi  Disemba mtendaji atakaeshindwa kutekeleza agizo hilo kwa asilimia atahesabika amepwaya na jumuiya iti tena 

Mapema Mwenyekiti ws UVCCM Wilaya ya Simanjiro Kiria Ole Laizer alisema ni wajibu wa kila mtendaji wa jumuiya hiyo kuelewa na kutambua mipaka na jukumu lake, kusimamia na kutekekza kwa maarifa na ufanisi.

Ole Laizer aisema jumuiya ya UVCCM ndiyo  moyo na shamba bora  linalotegemewa kutoa mavuno yenye tija kwa uongozi bora ambao utashika hatamu za utawala na kuendsha medani za madaraka kwa weledi, ujuzi, nidhu na maarifa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.