Habari za Punde

Uzinduzi wa mabaraza ya vijana Wilaya ya Magharibi A


Waziri Wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akihutubia wakati wa uzinduzi wa Baraza la Vijana la Wilaya ya Magharibi ‘A’ mjini kisiwani Zanzibar ambapo alkua Mgeni Rasmi.

Waziri Wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Magaharibi A Mh. Mwinyiusi Hassan wakati aliposhiriki uzinduzi wa baraza la vijana la wilaya hiyo kama Mgeni Rasmi.
Mgeni Rasmi katika uzinduzi wa Baraza la Vijana Wialaya Magharibi A, Waziri Wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Baraza hilo .

Mgeni Rasmi katika uzinduzi wa Baraza la Vijana Wialaya Magharibi A, Waziri Wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akionyesha cheti kama ishara ya uzinduzi wa Baraza la Vijana wilaya ya Magharibi A.

Mgeni Rasmi katika uzinduzi wa Baraza la Vijana Wialaya Magharibi A, Waziri Wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akifurahia jambo pamoja na Mbunge wa Jimbo la Mgharibi A, Mh Saada Mkuya, Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Bi. Farida Juma na Mkuu wa Wilaya ya Magaharibi ‘A” Mh Mwinyiusi Hassan.
Mgeni Rasmi katika uzinduzi wa Baraza la Vijana Wialaya Magharibi A, Waziri Wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akifurahia zawadi alizopatiwa na Braza la Vijana Wilaya ya Magharibi A.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. January Makamba amewataka vijana wasisite kuleta mabadiliko chanya katika Nchi mana Vijana ndiyo tegemeo la Taifa. Ameyasema hayo mjini Unguja alipokua akizindua Baraza la Vijana la Wilaya ya Magharibi A iliyoko mkoa wa …

Amewasishi Vijana watumie baraza hilo kama tanuri ya kutengenezea mbinu za uongozi na pia kama daraja la kuanzishia vikundi vya ujasiriamali na uzalshaji mali na kutengeneza njia mbalimbali za kuinua uchumi na kutowafanya kuwa tegemezi.

Akijibu risala ya Vijana hao ambayo imesomwa na Mwenyekiti wa Baraza hilo la Vijana Bi Farida Juma ambapo walitaja changamoto zinazowakabili ni pamoja na uhaba wa fedha, Waziri Makamba amelitaka Baraza hilo kufungua akaunti na yeye atawapatia mchango wake wa shilingi milioni mbili.

Awali akimkaribisha Mheshimwa Mgeni Rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Magaharibi A, Mheshimiwa Mwinyiusi Hassan amewataka vijana kuwa nguvu kazi ya Taifa na pia wahakikishe wanalinda na kuheshimu na kuulinda utamaduni wa Nchi yetu.

Wakitoa shukrani zao kwa Mgeni Rasmi Mwakilishi wa Baraza hilo la Vijana walimshukuru Mheshimiwa Waziri kwa kuitikia wito wao wa kumuomba awe mgeni Rasmi katika siku yao hiyo adhimu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.