Habari za Punde

Mchango wa mtoto Ummu Salama tayari Milioni tatu laki tatu na elfu 25 zimepatikana tuendelee kumchangia


Tunashukuru mpaka leo tumeweza kukusanya 3,325,000 , milioni 3 laki 3 na elfu 25.

Vilevile tunapenda kutangazia kwamba mchango huu utaendelea na hii ni kwasababu zifuatazo.

1. Baadhi ya Watu wameomba muda uongezwe ili na wao wapate kuchangia.

2. Kuna michango inayoendelea kwasababu kuna watu wengine wamechelewa kusikia habari hii.

3. Tuliwaomba viongozi wa dini wajaribu kulipeleka mbele suala hili na kuna wale ambao wameanza changamoto hio.

4. Ziko pesa ambazo zimesha changwa  lakini bado hazijatufikia mikononi mwetu.

5. Na la mwisho madhumuni ya Mchango huu ni kukusanya milioni 15 ili tumsafirishe mtoto Ummu Salama akapate matibatu yake.

Kutokana na sababu hizo napenda kuchukua nafasi ya kuwaomba  tena muzidi kujitokeza kwa wingi na kila mtu ajitahidi kwa upande wake kwa hali na mali mpaka tufanikiwe kwa uwezo wake Allaah Subhaanhu wata'ala


Kwa wale walioko UK unaweza kutuma mchango wako kupitia

Saba Traders Sort 090128  Account 78395061 (Santander)

Au wasiliana na Balozi mob 07846255735

Tafadhali unapochangia kwa kutumia akaunti weka ref Abuu Zam.

Vilevile nijuulishe kwa whatsapp +447947468729.

Kwa wale waliopo USA, Europe au Gulf unaweza kutuma kwa kupitia Western Union Anapokea Abuu Zam Tafadhali nijuulishe kwa  whatsapp +447947468729.

Kwa waliopo Tanzania nipigie simu kwa whatsapp au simu Zantel +255777917870.

Au unaweza kuwasiliana na mama wa mtoto na kumtumia moja kwa moja wasiliana nae kwa +255777257269.

Shime ndugu zangu tujitahidi kumsaidia mtoto huyu kwani Mtume Swalla Allaahu ‘alayhi Wasallam anasema Mwenye kumpunguzia Muislamu mwenzake mtihani katika mitihani ya kidunia, Allaah atampunguzia mitihani yake katika mitihani ya kidunia na akhera.Wabillaahi Tawfiyq.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.