Habari za Punde

Jengo Katika Mji Mkongwe laanguka na Kuuwa Mtu Mmoja leo mchana.

 Moja ya jengo katika mtaa wa hurumzi Unguja limeanguka wakati mafundi wakiwa katika kulifanyia ukarabati jengo hilo katika majira ya mchana saa 5, katika ajali hiyo mtu mmoja ambaye ni mmoja kati ya mafundi waliokuwa kazini katika jengo hulo amefariki dunia na mwengine kujeruhiwa baada ya kufunikwa na kifusi cha jengo hilo.
 Jengo hili lilikuwa katika matengenezo yake lilikuwa halikaliwa na watu, kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo wamesema jengo hilo lilikuwa katika harakati za ujenzi wake kwa kufunga majukwaa ya miti ili kutoa fursa kwa mafundi hao kulifanyia ukarabati. Katika ajali hiyo watu wawili ndio waliopata mkasa huo walikuwa ni mafundi na mtu aliyefariki dunia alitambuliwa kwa jina la Khamis Kombo mkaazi wa muembe makumbu unguja na mwezake alelazwa katika hospitali ya mnazi mmoja kwa matibabu akiwa katika hali mbaya baada ya kupata majaraha ya kufunikwa na kifusi cha jengo hilo. 
Sehemu ya kifusi cha jengo hilo kikiwa katika eneo la tukio katika mtaa wa hurumzi kwenda kwa jani jiranina kwa hassan mpiga picha. 
No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.