Habari za Punde

Kamati ya Baraza la Wawakilishi ya Mawasiliano na Ujenzi Yatembelea Miradi ya Ujenzi wa Barabara ya Kiwani -Likoni Pemba.

Wafanyakazi wa Idara ya Utunzaji Barabara Kisiwani Pemba wakiweka lami mpya barabara ya Mgagadu Kiwani -Likoni ikiwa katika hatua za mwisho ya ujenzi wa barabara hizo kisiwani Pemba ili kuimarisha miundombinu ya barabara kilichoombwa na Wananchi wa kiwani kuwekewa lami kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, wakati wa ziara yake hivi karibuni.
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Kamati ya Mawasiliano na Ujenzi wakitembelea barabara hiyo kujionea maendeleo yaliofikia katika uwekaji wa lami mpya.
WAJUMBE wa Kamati ya Mawasiliano na Ujenzi ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, wakimsikiliza Mzee Khamis Ali Khamis mkaazi wa nyumba za Maendeleo Kengeja, akitoa maelezo ya Nyumba hizo kwa wajumbe hao walipotembelea kuona hali ya nyumba hizo zilivyo
WAJUMBE wa Kamati ya Mawasiliano na Ujenzi ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, wakikagua ghala la shirika la bandari ya Mkoani wakati wa ziara yao walipotembelea bandarini hapo
MKURUGENZI mkuu wa Shirika la bandariu Zanzibar, Abdalla Juma akiwaonyesha mipaka ya eneo la shirika la bandari Mkoani, wajumbe wa kamati ya Mawasiliano na Ujenzi ya baraza la wawakilishi Zanzibar,wakati wapotembelea bandarini hapo.
(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.