Habari za Punde

Kamati ya Mawasiliano na Ujenzi ya Baraza la Wawakilishi wafanya ziara Pemba

 MKURUGENZI wa Idara ya Usafiri na Leseni Zanzibar, Suleiman Kirobo, akijibu hoja za wajumbe wa kamati ya Mawasiliano na Ujenzi ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, wakati walipotembelea Karakana Kuu ya Serikali iliyopo Tibirinzi Chake Chake Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA).
 BAADHI ya Vifaa vilivyomo katika Karakana kuu ya Serikali iliyopo Tibirinzi Chake Chake Pemba, vikilalamikiwa na wajumbe wa Kamati ya Mawasiliano na Ujenzi ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakiongozwa na Mhe:Hamza Hassan Juma, kutokana na uchakavu wake hali inayorudisha nyuma maendeleo ya Serikali.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA).

  BAADHI ya Vifaa vilivyomo katika Karakana kuu ya Serikali iliyopo Tibirinzi Chake Chake Pemba, vikilalamikiwa na wajumbe wa Kamati ya Mawasiliano na Ujenzi ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakiongozwa na Mhe:Hamza Hassan Juma, kutokana na uchakavu wake hali inayorudisha nyuma maendeleo ya Serikali.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA).
 MWENYEKITI wa Kamati ya Mawasiliano na Ujenzi ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mhe:Hamza Hassan Juma wa kwanza kushoto, kulia ni Naibu waziri wa Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar, Mhe:Mohamed Ahmad Salum, wakipitia Ripoti ya Mamlaka ya Uwanja wa Ndege wa Karume Pemba, baada ya kamati hiyo kutembelea Uwanja huo.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA).
 MAKAMU mwenyekiti wa Kamati ya Mawasiliano na Ujenzi ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, mwakilishi wa jimbo la Chake Chake Mhe:Suleiman Sarahan Said, akiuliza swali kwa wakurugenzi wa Malaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar, wakati kamati hiyo ilipotembelea uwanja wa wa Ndege wa Karume Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA).
 MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar Saidi Iddi Ndubugani, akitoa maelezo kwa wajumbe wa kamati ya Mawasiliano na Ujenzi ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar,wakati walipotembelea uwanja wa Ndege wa Karume Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA).

MWENYEKITI wa Kamati ya Mawasiliano na Ujenzi ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, ambaye ni mwakilishi wa Jimbo la kwa Mtipura, Mhe:Hamza Hassan Juma, akiangalia ramani ya uwanja wa Ndege wa Karume Kisiwani Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA).

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.