Habari za Punde

Mwandishi wa habari za michezo, gazeti la uhuru Amina Athumani afariki dunia asubuhi hii katika Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar.

Mwandishi Amina enzi za uhai wake

Innaa Lillaahi wainnaa ilayhi raajiuun

Mwandishi wa habari za Michezo wa Gazeti la Uhuru, Amina Athuman (pichani) amefariki Dunia leo asubuhi katika Hosptali ya Mnazi Mmoja mjini Zanzibar alikokuwa amelazwa.

Amina alilazwa Hospitalini hapo baada ya kuzidiwa (kushikwa na uchungu) kutokana na ujauzito na kukimbizwa kupata huduma katika hospitali hiyo ambpo alijifungua mtoto wa Kiume (Bahati mbaya) na yeye akaendelea kupatiwa matibabu hadi yalipomkuta umauti asubuhi ya leo.

Amina alikuwa mjini Zanzibar kikazi alipokwenda kuripoti mashindano ya Kombe la Mapinduzi, ambapo alikuwa arejee jijini Dar es Salaam jana.

Mungu ailaze roho ya Marehemu Amina Athuman mahala pema peponi, Amina

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.