Habari za Punde

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Magufuli Afungua Viwanda Viwili Mkoani Shinyanga.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli akikata utepe kuashiria kufungua rasmi Kiwanda cha kutengeneza mifuko ya Sandarusi cha Fresho Investment Company limited cha Mkoani Shinyanga. Wengine katika picha ni mkuu wa mkoa wa Shinyanga  Zainabu Taleck wakwanza kulia mwenye kilemba , mbunge wa Shinyanga mjini Stephen Masele wakwanza kushoto, pamoja na mmiliki wa kiwanda hicho Fred Shoo watano kutoka kulia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli akivuta utepe kwenye jiwe la ufunguzi wa kiwanda hicho cha kutengeneza mifuko ya Sandarusi cha Fresho Investment Compaany limited cha Mkoani Shinyanga. Kulia ni mmiliki wa Kiwanda hicho Fred Shoo.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli akimsikiliza mmiliki wa wa kiwanda hicho cha Fresho,  Fred Shoo kuhusu malighafi ya kutengenezea mifuko ya Sandarusi. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.