Habari za Punde

Rais wa Zanzibar Dk Shein Awaapisha Viongozi Aliowateua.

STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
  Zanzibar                                                        23.1.2017
---
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein leo amewaapisha viongozi aliowateua hivi karibuni kushika nyadhifa mbali mbali katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Viongozi walioapishwa na Rais Dk. Shein katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar ni Dk. Sira Ubwa Mamboya ambaye anakuwa Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na Waziri asiekuwa na Wizara Maalum.

Wengine ni Bi Zainab Omar Mohammed ambaye anakuwa Mshauri wa Rais wa Masuala ya Jamii, Wazee, Wanawake na Watoto, Dk. Maua Abeid Daftari anakuwa Mshauri wa Rais- Pemba na Bi Rahma Ali Khamis ambaye anakuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.

Hafla hiyo, ilihudhuriwa na viongozi mbali mbali akiwemo Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd,  Spika wa Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali Maulid, Jaji Mkuu wa Zanzibar  Omar Othman Makungu, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Said Hassan Said, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Issa Haji Gavu.

Viongozi wengine waliohudhuria hafla hiyo ni Mawaziri wasio na Wizara Maalum ambao pia, ni Wajumbe wa Baraza la Mapinduzi, Naibu Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto Shadya Mohamed Suleiman, Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabih, Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji.

Na wengine ni Mkuu wa  Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud, Meya wa Manispaa ya Mji wa Zanzibar Khatib Abrahman Khatib, Washauri wa Rais wa Zanzibar pamoja na viongozi wengine wa Serikali.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 
 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.