Habari za Punde

Wakuu wa Mashirika ya Umeme Kutoka Nchi Kumi za Eastern Africa Wakutana Arusha Kujadili Namna ya Kuunda Mifumo ya Usafirishaji Umeme Kwa Nchi Hizo.


Na Woinde Shizza,Arusha


Wakuu wa  Mashirika ya Umeme kutoka katika Nchi kumi za Afrika zinazozalisha
Umeme(Eastern Africa Power pool(EAPP)          zimekutana  jijini Arusha kwa malengo ya kujadili mfumo wa usafirishaji wa umeme ikiwa ni pamoja na namna ya wananchi wao watakavyoweza pata nishati ya umeme kwa uraisi tofauti
na sasa.

Hayo yalisemwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Dkt.Juliana Palangyo alipokuwa akizungumza katika ufunguzi wa mkutano huo  wa Wakuu wa Mashirika ya Umeme katika Nchi hizo za Eastern Africa Power Pool (EAPP) mapema leo.

Dkt.Palangyo alisema kuwa lengo halisi ni kuweza kujadili mambo mbalimbali yahusuyo na nishati ya umeme kwa watumiaji wake kwani  kuna uwezekano  mkubwa wa nchi zote zilizo kwenye umoja huo.

Alisema kwa sasa yapo baadhi ya makampuni ambayo yalikuwa yanauza umeme kwa gharama kubwa hasa kwa wananchi ambao hawajapata huduma hiyo ya umeme lakini kupitia umoja huo wataweza kupata nishati hiyo kwa gharama nafuu.

"Hizi nchi za eastern tumekutana hapa ili tujadili namna ambayvo tunayvoweza kutafuta namna ya kuzalisha umeme kwa bei nafuu na kisha nchi hiyo itaweza kuuza umeme  kwa bei ndogo"aliongeza Dkt.Palangyo.

Hata hivyo kwa upande Kaimu Meneja Uhusiano wa Shirika la Tanesco Bi.leila Muhaji alisema kuwa katika mkutano huo pia watajadili namna ambavyo Tanzania itajenga njia ya usafirishaji wa umeme wa njia ya maji ambayo itatoka nchi ya Tanzania kwendas Kenya,Zambia,pamoja na nchi nyingine

Muhaji alisema kuwa Tanzania itanufaika na ujenzi wa njia hizo hivyo jamii itanufaika kwa kiwango kikubwa sana kama ilivyo kwenye nchi ambazo zimeendelea duniani.

"Hata hivyo mara baada ya huu mkutano wa wakuu wa nchi zinazolisha umeme tunatarajia pia kuwepo na wadau wengine ambao ni mawaziri kutoka nchi zote ambao nao sasa wataweza kuweka mambo sawa ili huduma hii iweze kumfikia mlengwa"aliongeza Muhaji

Alimalizia kwa kutaja nchi ambazo zina unda umoja huo kuwa ni  Tanzania ,Kenya,Uganda ,Rwanda ,Burundi ,Sudan , Congo, Ethiopia ,Djbout, Libya pamoja na Egypt.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.