Habari za Punde

Zantel Yaipiga Jeki Jeshi la Polisi Usalama Barabarani Zanzibar Laipatia Vifaa vya Mawasiliano

Mkuu wa Masoko wa Kampuni ya Zantel Mohammed Mussa Baucha akimkabidhi vifaa vya mawasiliano Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe, Ayoub Mohammed Mahmoud, ikiwa ni katika jitihada za kuendeleza Uzinduzi wa Mabalozi wa Usalama Barabarani,hafla hiyo imefanyika katika Afisi ya Mkuu wa Mkoa Vuga Zanzibar. Kampuni ya Zantel imekabidhi Ipad 12 kwa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Kanda ya Zanzibar kufanikisha Mtandao huu wa Mabalozi wa Usalama barabarani kupokea taarifa kutoka kwa wananchi kupitia mitandao hiyo kupunguza ajali za barabarani Zanzibar.     
Mkurugenzi wa Masoko Kampuni ya Zantel Mohammed Mussa Baucha akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa vya mawasiliano kwa ajili ya Jeshi la Polisi Usalama Barabarani kutumika kupunguza ajali za barabarani kutoa taarifa kwa jeshi hilo kupitia vifaa hivyo.kwa wananchi wanapoona madereva wanahatarisha usalama wa abiria, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Vuga.  
Mkurugenzi Masoko wa Kampuni ya Zantel akisisitiza jambo wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi Ipad 12 kwa Jeshi la Polisi Zanzibar Usalama Barabarani. na kusema Ipad hizo zitakuwa na 10GB kila mwezi ili kuweza kuwasiliana na wananchi kupokea taarifa ya uhalifu wa barabarani.  
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe Ayuob Mohammed Mahmoud akimkabidhi DCP Juma Msige vifaa hivyo vya mtandao kutrahisisha mawasiliano kwa Jeshi la Polisi Usalama Barabarani kupokea taarifa za uhalifu wa barabarani kupitia mitandao hiyo iliotolewa na Kampuni ya Zantel  
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mohmoud akizungumza wakati wa hafla hiyo na kutowa shukrani kwa kampuni ya Zantel kwa msaada wake huo wa vifaa vya mawasiliano kwa Jeshi la Polisi Usalama Barabarani kudhibiti ajali za barabarani kwa kupokea Taarifa kutokwa kwa wananchi wakati wa kutokea uhalifu wa kiusalama barabarani Zanzibar. 
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo wa makabidhiano ya Vifaa vya mawasiliano kwa Jeshi la Polisi Usalama Barabarani Kanda ya Zanzibar.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mohmoud akizungumza wakati wa hafla hiyo na kutowa shukrani kwa kampuni ya Zantel kwa msaada wake huo wa vifaa vya mawasiliano kwa Jeshi la Polisi Usalama Barabarani kudhibiti ajali za barabarani kwa kupokea Taarifa kutokwa kwa wananchi wakati wa kutokea uhalifu wa kiusalama barabarani Zanzibar. 
 DCP Juma Msige, akitowa shukrani kwa kampuni ya Zantel kwa msaada wao wa vifaa vya mawasiliano kwa ajili ya matumizi ya Jeshi la Polisi Usalama Barabarani Zanziba.r 


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.