Habari za Punde

Maandalizi ya kusambaza umeme kisiwa cha Fundo

 MAFUNDI wa shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) Tawi la Pemba, wakiteremsha nguzo za umeme kutoka katika meli ya Mv Jitihada, iliyofunga nanga katika kisiwa cha Fundo, kwa ajili ya huduma hiyo kupelekwa katika kisiwa Hicho.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
 MAFUNDI wa Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) Tawi la Pemba, wakibeba nguzo za umeme kutoka katika meli ya Mv Jitihada, iliyopo katika kisiwa cha Fundo na kuzipeleka juu katika kisiwa hicho, kwa ajili ya kupelekwa umeme kisiwani huko.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

 BAADHI ya Mafundi wa shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) Tawi la Pemba, wakitoa maringi yaliyohifadhiwa waya wa umeme katika meli ya MV Jitihada na kuvipeleka katika kisiwa cha Fundo, baada ya meli hiyo kufika kisiwani huko na vifaa mbali mbali kwa ajili ya kusambaza umeme.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

WAFANYAKAZI wa Shirika la umeme Zanzibar (ZECO) Tawi la Pemba, wakiiteremsha moja ya Tansfoma inayotaka kuwekwa katika kisiwa Cha Fundo, kutoka katika gari maalumu uliyoibeba kutoka ndani ya Meli ya MV Jitihada, iliyofika katika bandari ya fundo kwa kuteremsha vifaa mbali mbali vya Umeme Kisiwani huko.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.