Habari za Punde

Matembezi ya Shamrashamra ya Wiki ya Sheria Zanzibar.

Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe Mwanajuma Majid na Watendaji wa Mahakama Maofisa Wadhamini na Wananchi Kisiwani Pemba wakishiriki katika Matembezi ya Maalum ya kuadhimisha Siku ya Sheria  matembezi hayo yameazia katika Afisi ya Mahakama Kuu Pemba na kumalizikia katika Viwanja vya  michezo Gombani Chakechake yakiwa ya kilomita Tatu. 





Watendaji wa Mahakama Pemba na Maofisa wa Serikali wakishiriki katika mchezo wa kuvuta kamba ikiwa ni shamrashamra za Wiki ya Sheria. 
Washindi wa mchezo wa kuvuta kamba ambao  ni Jeshi la Polisi, waliowavuta watendaji wa mahakama, wateule wa rais, waendesha mashitaka na wanasheria wengine, ikiwa ni sehemu ya shamra shamra kuelekea siku ya sheria duniani, ambapo inatarajiwa kuadhimishwa Febuari 9 mwaka huu
Wafanyakazi wa Afisi ya Mahakama Kisiwanin Pemba wakishiriki katika mchezo wa uvutaji wa kamba na Askari ya Jeshi la Polisi Pemba, wakati wa matembezi ya Wiki ya Sheria yaliofanyika katika viwanja vua mpira gombani Chakechake Pemba, Maadhimisho yake yatafanyika tarehe 9 febuary 2017. 
Mrajisi wa Mahakama Kuu Pemba Mhe. Hussein Makame Hussein akizungumza wakati wa shamrashamra za kuadhimisha Wiki ya Sheria ilioaza kwa matembezi na kuwashirikisha Watendaji mbalimbali, matembezi hayo yameishia katika viwanja vya mpira gombani na kufanya mazoezi na ufutaji wa kamba.
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe.Mwanajuma Majid Abdalla, akizungumza kwenye shamra shamra za kuelekea siku ya sheria, kwenye uwanja wa michezo Gombani Chakechake Pemba, ambapo kabla Mkuu huyo wa Mkoa aliongoza matembezi, yalioanzia mahakama kuu na kuishia uwanjani hapo, (Picha na Haji Nassor, Pemba).

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.