Habari za Punde

Mawaziri wa Zanzibar watembelea Wizara ya Ardhi ya SMT kwa ajili ya kubadilishana uzoefu

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe William Lukuvi akiwaelezea Mawaziri kutoka Zanzibar jinsi Kituo cha Huduma kwa Mteja cha Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kinavyorahisisha kutoa Huduma za Ardhi bila usumbufu kwa Wananchi. Kuanzia Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe. Mohamed Aboud, Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar Mhe. Hamad Rashid, Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira Zanzibar Mhe. Salama Talib na Katibu Mkuu Wizara wa Ardhi Dkt. Yamungu Kayandabila.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe William Lukuvi akimuonesha Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe. Mohamed Aboud jinsi ya kutumia mashine ya kutolea huduma za Ardhi katika kituo cha Huduma kwa Mteja cha Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira Zanzibar Mhe. Salama Talib akipata maelezo kutoka kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe William Lukuvi jinsi Wizara yake ilivyofanikiwa kuyapatia ufumbuzi masuala mbalimbali ya Ardhi na kuwaondolea usumbufu Wananchi katika kupata huduma za Ardhi. Kushoto ni Katibu Mkuu Wizara wa Ardhi Dkt. Yamungu Kayandabila. 
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe William Lukuvi akiwa na ujumbe wa Mawaziri kutoka Zanzibar walipofika ofisini kwake.
Wananchi wakipata Huduma za Ardhi katika Kituo cha Huduma kwa Mteja cha Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.