Habari za Punde

Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Zanzibar Mhe. Mohammed Raza Azungumza na Waandishi wa Habari Zanzibar.

Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Zanzibar Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja Mhe Mohammed Raza akizungumza na waandishi wa habari utekelezaji wa Ilani ya CCM na ahadi za Wananchi wake alizoahidi jinsi anavyoendelea kuzitekeleza ikiwa ni shamrashamra za miaka 40 ya Chama Cha Mapinduzi, na kuwashukuru wapiga kura wake Wananchi wa Uzini Zanzibar.
Na kutowa shukrani kwa wananchi hao kwa ushirikiano wao na kufanikisha sehemu kubwa za ahadi zake na kuendelea kuleta maendeleo katika jimbo hilo. 
 Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mhe Mohammed Raza akisisitiza jambo wakati akijibu maswali aliyokuwa akiulizwa na waandishi wa habari kuhusiana na utekelezaji wa ahadi zake kwa Wananchi wa Uzini Zanzibar. na kuelezea amatekeleza miradi mingi katika jimbo lake.  
Mhe Raza akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo yake na waandishi wa habari katika ukumbi wa hoteli ya Grand Palace Malindi Zanzibar.
 Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar wakifuatilia mkutano huo na Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Zanzibar Mhe Mohammed Raza uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Grand Palace Malindi Zanzibar. 
No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.