Habari za Punde

Rais Dk Shein afanya uteuzi wa Katibu Mkuu na manaibu Katibu

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, jana tarehe 3 Febuari, 2017 amefanya uteuzi wa viongozi katika taasisi mbalimbali za Serikali kama ifuatavyo:

1. KATIBU MKUU WA WIZARA YA AFYA:


Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 50 (2) na (3) cha Katiba ya Zanzibar ya 1984, Rais amemteua Bibi Asha Ali Abdulla kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya.
Aidha kwa mujibu wa kifungu cha 12 (3) cha sheria ya Utumishi wa Umma Namba 2 ya 2011, Rais Dk. Shein ametengua uteuzi wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dk. Juma Malik Akili na atapangiwa kazi nyengine.

2. KATIBU MKUU WA OFISI YA RAIS, KATIBA, SHERIA , UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA:

Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 50 (2) na (3) cha katiba ya Zanzibar ya 1984, Rais amemteua Bwana Yakout Hassan Yakout kuwa Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

3. NAIBU KATIBU MKUU WA OFISI YA RAIS, KATIBA, SHERIA, UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA ANAYESHUGHULIKIA UTUMISHI WA UMMA:

Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 50 (4) cha katiba ya Zanzibar ya 1984, Mhe. Rais amemteua Bwana Seif Shaaban Mwinyi kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora anayeshughulikia Utumishi wa Umma.

Uteuzi huo umeanza  tarehe 3, Febuari, 2017.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.