Habari za Punde

Siku ya Sheria ni Siku Ambayo Wananchi Hupata Msaada wa Kisheria

Wakili wa kujitegemea Mruma aShabibu kutoka kampuni  IRM Legal  alisema kuwa siku hii ni maalum kwa mawakili kutoa huduma za kisheria kwa jamii bila malipo yeyote.

Na Pamela Mollel,Arusha
Imeelezwa kuwa siku ya sheria ni siku ambayo wananchi wanapata fursa ya kupata msaada wa kisheria ambayo kila mwananchi anapaswa kuwa chini ya sheria na sio juu ya sheria.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake wakili wa kujitegemea Mruma Shabibu kutoka kampuni  IRM Legal  alisema kuwa siku hii ni maalum kwa mawakili kutoa huduma za kisheria kwa jamii bila malipo yeyote.

Alisema kuwa siku hii watu wengi hufaidika kwa kutatuliwa baadhi ya matatizo yao bila kutozwa gharama yeyote ikiwa ni pamoja na kupata elimu ya kisheria sanjari na kupata fursa ya kubadilishana mawazo na mawakili.

Alidai kuwa wananchi wanapaswa kuheshimu katiba lakini pia na kukaa chini ya sheria ili haki iweze kutendekea kwani baadhi ya wananchi wanakaa juu ya sheria hali ambayo inawafanya kujiona hawatendewi haki.

Hata hivyo alifafanua kuwa lengo la kuanzishwa kwa siku hii ni kuangalia umuhimu wa sheria katika jamii na kuona jinsi inavyofanya kazi katika kukuza uchumi wa nchi 


Wakili wa kujitegemea Mruma aShabibu kutoka kampuni  IRM Legal  alisema kuwa siku hii ni maalum kwa mawakili kutoa huduma za kisheria kwa jamii bila malipo yeyote.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.