Habari za Punde

Tuvienzi vyetu vya Asili - Resi za Ngarawa


Resi za ngarawa ingawa wengine huiita ngalawa ni miongoni mwa vivutio vya kihistoria katika visiwa vya Zanzibar. 

Katika miaka ya zamani resi za ngarawa zilikuwa ni mojawapo katika mambo yanayofanyika kila mwaka kwenye shamra shamra za sherehe za Mapinduzi na hufanyika maeneo ya Forodhani jirani na Mambo Msiige (Sasa Park Hyatt) na hoteli ya Tembo.

Kulikuwa na ngarawa mahasimu kati ya Malindi na Hidaya ambapo walikuwa wakipokeza ushindi huku tukiwasubiri kwa hamu wakienda kugeuza kwenye kisiwa mojawapo.

Siku hizi resi hizi zimesahauliwa ingawa kuna sehemu nyengine wameanza kuzifufua kama kisiwani Pemba ambapo karibuni walifanya resi za ngarawa Vuma wimbi na kama Mwakilishi wa Tunguu Simai Mohammed Said alipozindua resi hizi jimboni kwake. 

Picha isiyokuwa na rangi ni kwa hisani ya Narendra Gajjar


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.