Habari za Punde

Ubalozi wa Uswiss Wachangia Tamasha la Sauti za Busara Zanzibar.

Balozi wa  Uswiss Nchini Tanzania Balozi Tinguly Mattli akimkabidhi mfano wa cheki ya shilingi milioni 260 Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Sauti za Busara Zanzibar Mhe, Simai Mohammed Said, hafla hiyoo ya makabidhiano imefanyika katika ukumbi wa Ofisi za Ubaloai wa Uswiss Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Sauti za Busara Zanzibar Mhe  Simai Mohammed Said akizungumza na Balozi wa Uswiss Nchini Tanaznia  Mhe. Tinguely Mattli wakati wa hafla ya makabidhiano ya Cheki kusaidia Tamasha la Sauti za Busara Zanzibar kwa kipindi cha miaka mitatu, kufanikisha Tamasha hilo la Muziki kuendesha shughuli zake za kuitangaza Zanzibar katika Utalii  
Balozi wa Uswiss Nchini Tanzania   Mhe. Tinguely Mattli (kulia) akizungumza na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Sauti za Busara Zanzibar, Mhe. Simai Mohammed Said na kushoto  Bi. Romana Tedeschi wakati wa hafla hiyo iliofanyika katika ukumbi wa Ubalozi wa Uswiss Jijiji Dar es Salaam.

Ubalozi wa Uswisi Nchini umechangia zaidi ya shilingi milioni 260 ili kuwezesha Tamasha la Muziki la Sauti za Busara Zanzibar kwa miaka mitatu ijayo. Balozi wa Uswisi nchini Tanzania, Mhe. Florence Tinguely Mattli, akizungumza na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Busara Promotions Mhe. Simai Mohammed Said kwa ajili ya makabidhiano katika ofisi za Ubalozi jijini Dar es Salaam.

Sauti za Busara ni kati ya matamasha ya muziki yanayoheshimika sana barani Afrika. Tamasha hili la kipekee linahamasisha kuheshimu tofauti kati ya watu kwa kuleta watu pamoja kusherehekea muziki ‘live’ kutoka Barani la Afrika. Lengo la tamasha hili ni kuongeza ujulikanaji na upatikanaji kwa muziki wa Afrika, kuendeleza ujuzi na fursa kwa ajili ya wale walio katika sekta ya muziki na kuimarisha ushirikiano na mitandao ya muziki kikanda na kimataifa.
"Uswisi imekuwa ikisaidia matukio na juhudi mbalimbali katika sekta ya sanaa na utamaduni nchini Tanzania kwa zaidi ya miaka kumi sasa," alisema Balozi Tinguely Mattli. "Tamasha la Sauti za Busara ni mfano mzuri wa tukio kitamaduni ambalo huleta watu pamoja ili kufurahia kazi za sanaa na wakati huo huo kuchangia maendeleo ya kiuchumi."
Mheshimiwa Simai alitoa shukrani kwa niaba ya Bodi ya Wadhamini ya Busara Promotions kwa msaada huo. "Mashirika ya sanaa na utamaduni yanategemea sana ufadhili wa wadau wa maendeleo. Tunashukuru Ubalozi wa Uswisi kwa mchango wao katika kuwezeshaea kufanikisha tamasha hili," alisema.

Tamasha la Sauti za Busara litaanza tarehe 9 na kufikia tamati tarehe 12 Februari 2017 katika ukumbi wa kihistoria wa ‘Old Fort’ mjini Stone Town, Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.