Habari za Punde

Wajumbe wa kamati ya katiba, sheria na utawala BLW ziarani Pemba

 WATENDAJI wakuu wa wizara inayoshughulikia Utumishi wa Umma na Utawala bora Pemba, wakipitia ripoti ya robo mwaka, mara baada ya kusomwa na Afisa Mdhamini wa wizara hiyo Massoud Ali Mohamed, mbele ya wajumbe wa kamati ya katiba, sheria na utawala ya baraza la wawakilishi, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
 WAJUMBE wa kamati ya Katiba, sheria na utawala ya baraza la wawakilishi, wakisikiliza uwasilishaji wa ripoti ya robo mwaka ya wizara inayoshughulikia Utumishi wa Umma na utawala bora Pemba, wakati kamati hiyo ilipotembelea ofisi hiyo, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
 MWANASHERIA dhamana wa afisi ya Mkurugenzi wa mashitaka Pemba, Ali Rajab akiwasilisha ripoti ya robo mwaka ya afisi hiyo, mbele ya wajumbe wa kamati ya Katiba, sheria na utawala ya baraza la wawakilishi, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
 HAKIMU wa mahakama ya wilaya Wete Taki Abdalla Habib, akitoa maelezo kwa wajumbe wa kamati ya katiba, sheria na utawala ya baraza la wawakilishi wakati walipotembelea ofisi hiyo, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
 MWENYEKITI wa Kamati ya Katiba, sheria na Utawala ya baraza la wawakilishi, Machano Othaman Said, akizungumza kwenye kikao cha kupokea ripoti ya robo mwaka ya wizara inayoshughulikia utumishi wa umma na utawala bora Pemba, wakati kamati hiyo ilipotembelea kwenye ofisi hiyo, (Picha na Haji Nassor, Pemba).

 MDHAMINI wa mamlaka ya kuzuia rushwa na uhujumu wa uchumi wa Zanzibar ‘ZAECA’ ofisi ya Pemba Suleiman Ame Juma, akitoa ufafanuzi wa kazi za mamlaka hiyo, mbele ya wajumbe wa kamati ya katiba, sheria na utawala ya baraza la wawakilishi Zanzibar, wakati ilipofika kwenye ofisi hiyo mjini Chakechake, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
AFISA Mdhamini wa wizara inayoshughulikia utumishi wa umma na utawala bora Pemba, Massoud Ali Mohamed, akiwasilisha ripoti ya kazi ya robo mwaka ya wizara yake, mbele ya wajumbe kamati ya katiba, sheria na utawala ya baraza la wawakilishi walipofika wizarani hapo, kupata taarifa hiyo, kabla ya kuzitembelea Idara zilizomo ndani ya wiara hiyo, (Picha na Haji Nassor, Pemba).  

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.