Habari za Punde

Benki ya Watu wa Zanzibar PBZ Yakabidhi Msaada wa Mabati Kwa Ajili ya Ujenzi wa Madrasatul Tarbbiyya Islamia Kigongoni Kijiji cha Fukuchani Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Meneja Masoko wa Benki ya Watu wa Zanzibar Mohammed Nuhu akiondoa kipazia kuashiria kuweka jiwe la Msingi la Madrasatul Tarbbiyya Islamia ya Kinongoni Fukuchani Wilaya ya Kaskazini A Unguja na kukabidhi msaada wa mabati 173 kwa ajili ya ujenzi wa madrasa hiyo ya kisasa katika Kijiji hicho na kutowa elimu kwa Watoto wa Kijiji hicho. 
Muonekano wa Michoro ya majengo ya kisasa ya Madrasatul Tarbbiyya Islamia baada ya kukamilika kwa ujenzi wake ndivyo itakavyokuwa Inshaallah mwenyenzi mungu awaongoze kuweza kumalizia jengo hilo kwa ajili ya kutowa elimu ya maandalizi na dini watoto wa kijiji hicho. Wananchi litakalo mgusa hili anaweza kuchangia ili kuweza kufanikisha hili kwa ajili ya Watoto Wetu kupata Elimu Bora kwa Maisha yao na familia yao.


Msimamizi wa Ujenzi wa Madrasatul Tarbbiyya Islamia Kinongoni Fukuchani Zanzibar akitowa maelezo ya Ujenzi huo kwa Uongozi wa Benki ya Watu wa Zanzibar PBZ wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa mabati kwa ajili ya ujenzi huo.
Meneja Masoko wa Benki ya Watu wa Zanzibar Ndg Mohammed Nuhu akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa kwa ajili ya ujenzi wa Madrasatul Tarbbiyya Islamia Kinongoni Fukuchani Zanzibar, na kutowa shukrani kwa Uongozi wa Madrasa hiyo kwa juhudi zao kuweza kufanikisha kuanzisha mradi huo wa ujenzi wa madrasa ya kisasa katika kijiji chao kwa kuwa kijiji cha mfano baada ya kukamilika ujenzi huo.  
Wanafunzi wa madrasa hio wakifuatilia hafla hiyo.

Wazee na Walimu wa madrasa hiyo wakifuatilia hafla hiyo ya kukabidhi msaada wa mabati kutoka PBZ. hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya madrasa hiyo kinongoni fukuchani.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.