Habari za Punde

Mahafali ya Pili ya Chuo cha Waandishi wa Habari TSJ Tawi la Pemba Katika Ukumbi wa Kiwanda cha Makonyo Chakechake.

Viongozi wa Chuo cha TSJ na viongozi wengine wakiwa katika ukumbi wa hafla ya mahafali ya Chuo cha Waandishi wa Habari Tawi la Pemba yaliofanyika katika ukumbi wa ZSTC Makonyo Chakechake. 
Viongozi mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, wakifuatilia kwa makini mahafali ya Pili ya wahitimu wa fani ya Habari ngazi ya Cheti na Diploma katika Chuo cha Uwandishi wa Habari TSJ Tawi la Pemba, mahafali hayo yaliyofanyika huko katika ukumbi wa Makonyo Wawi Chake Chake
Mhitimu wa Fani ya Habari ngazi ya Cheti kutoka Chuo cha Uwanidshi wa habari Time School and Journalism (TSJ) Tawi la Pemba, Moza Abdi akisoma risala ya wafanuzi wakati wa mahafali ya pili ya Chuo hicho kufanyika Kisiwani Pemba
Mkuu wa Chuo cha Uwandishi wa habari Time School and Journalism (TSJ)Tawi la Pemba, Suleiman Rashid Omar akisoma risala ya Chuo wakati wa mahafali ya Pili ya chuo hicho kufanyika Kisiwani Pemba
Mkurugenzi wa Bodi ya Chuo cha Time School and Journalism Tanzania bara, Kiondo Mshana akitoa salamu za Chuo kwa wahitimu wa Fani ya Habari ngazi ya Cheti na Diploma, wakati wa mahafali ya pili ya chuo hicho kufanyika kisiwani Pemba
Afisa Mdhamini Wizara ya Habari Pemba, Khatib Juma Mjaja akitoa salamu zake kwa wahitimu wa fani ya habari ngazi ya Cheti na Diploma, wakati wa mahafali ya Pili ya Chuo cha Uwandishi wa Habari cha Time School and Journalism (TSJ) kufanyika Pemba
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya Zanzibar, Mhe:Harusi Said Suleiman, akizungumza na wahitimu wa fani ya habari ngazi ya Cheti na Diploma, wakati wa mahafali ya Pili ya Chuo cha Time School and Journalism (TSJ) Tawi la Pemba kufanyika Kisiwani Pemba
Wahitimu wa Fani ya Habari ngazi ya Diploma katika Chuo cha Uwandishi wa habari Time School and Journalism Tawi la Pemba, wa kwanza kushoto Zuhura Juma Said, Zuhura Msabah, Said Abrahman, ambao wanajitolea katika gazeti la Zanzibarleo Ofisi ya Pemba
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya Zanzibar Mhe:Harusi Said Suleiman, akimkabidhi cheti cha uwandishi wa habari ngazi ya Diploma, mhitimu Said Abrahman, ambaye anajitolea katika gazeti la Zanzibarleo Ofisi ya Pemba
Wahitimu wa Fani ya Habari Ngazi ya Cheti na Diploma, kutoka katika Chuo cha Time school and Journalism (TSJ) Tawi la Pemba, wakiwa katika mahafali yao ya Pili kwa Chuo hicho kufanyika Kisiwani Pemba.
Wahitimu wa Fani ya Habari Ngazi ya Cheti na Diploma, kutoka katika Chuo cha Time school and Journalism (TSJ) Tawi la Pemba, wakiwa katika mahafali yao ya Pili kwa Chuo hicho kufanyika Kisiwani Pemba.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA.)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.