Habari za Punde

Nasiha za Bi Hekima: Tusameheyane

Na Bi Hekima

Tuna kawaida ya kutumiana dua na aya siku za Ijumaa kama ukumbusho na kupeana salama za Ijumaa. 

Baadhi huona hii ni sadaka na utamaduni huu umezidi tokea mwezi wa Rajab uingie na bila shaka itadumu mpaka kukamilisha Ramadhan. 

Sadaka yangu mimi ni ukumbusho wa umuhimu wa kusisitiza kuwa watu (sisi) wawaombe msamaha wanaowakosea (kwa kukusudia au kwa kuteleza maana tunakazana na maghfira tu)...huo ndio uungwana na ucha mungu wa uhakika. 

Tunamkosea Jalali na tukimuomba msamaha na maghfira hutusamehe, na tunawakosea wengine...kila mmoja anastahili 'sorry' yake kwa kadri ya alivyokosewa. 

Na kama mimi nimekukosea, kwa hali yoyote, nisamehe

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.