Habari za Punde

Rais Dkt.John Pombe Magufuli Afungua Jengo la Ofisi ya Benki Kuu (BOT) Pamoja na Nyumba za NHC Mkoani Mtwara.

Sehemu ya Nyumba hizo za Ghorofa za Shirika la Nyumba la Taifa NHC katika eneo la Raha Leo mkoani Mtwara. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Profesa  Beno Ndulu, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Halima Dendego akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Jengo la Ofisi ya kutoa Huduma za Benki Kuu ya Tanzania Tawi la Mtwara


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi kabla ya kufungua rasmi Jengo la Ofisi ya kutoa Huduma za Benki Kuu ya Tanzania Tawi la Mtwara.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza  Mbunge wa Mtwara mjini kupitia Chama cha Wananchi (CUF) Maftah Nachuma kabla ya kufungua rasmi Nyumba za Shirika la nyumba la Taifa NHC katika eneo la Raha leo mkoani Mtwara.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Profesa  Beno Ndulu mara baada ya kufungua jengo la Ofisi ya kutoa Huduma za Benki Kuu ya Tanzania Tawi la Mtwara.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na baadhi ya watoto  mkoani Mtwara waliomfata kumsalimia mara baada ya kufungua jengo la Ofisi ya kutoa Huduma za Benki Kuu ya Tanzania Tawi la Mtwara.
Picha na Ikulu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.