Habari za Punde

Waandishi wa habari watembelea na kukagua miradi ya utafiti wa umeme wa nishati mbadala

 Mkuu wa Mawasiliano wa mradi wa nishati mbadala Zanzibar, Ndugu Sebastian Sanga akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) namna ya kujikita katika taarifa zenye changamoto katika jamii hapo katika ofisi za Shirika la Umeme (ZECO) Saateni mjini Unguja.
  Meneja wa mradi wa nishati mbadala Zanzibar, Bw. Maulid Shirazi Hassan akizungumza na waandishi wa habari katika mnara wa kufanyia utafiti nishati ya umeme mbadala hapo Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja juu ya maendeleo ya kazi ya utafiti wa nishati mbadala ya umeme Zanzibar.
 Ni sehemu ambayo mnara wa kuchukulia taarifa (nyuma ni mnara wa utafiti) za utafiti wa umeme wa nishati mbadala Makunduchi Mkoa Kusini Unguja
 Meneja wa mradi wa nishati mbadala Zanzibar, Bw. Maulid Shirazi Hassan akizungumza na waandishi wa habari katika kituo cha kupokelea umeme Fumba Zanzibar
 Baadhi ya waandishi wa habari wakipata maelezo ya namna ambavyo kituo kikuu cha  kupozea umeme Mtoni mjini Unguja kinavyofanya kazi. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.