Habari za Punde

FUFA Wawapa Kitendawili Marais wa CECAFA

Rais wa Shirikisho la Mpira wa miguu nchini Uganda (FUFA) Moses Magogo aliwapa mtihani wa kiutendaji marais wenzake wa CECAFA baada ya kutembelea jengo la ofisi za Shirikisho hilo wiki iliyopita.

Marais hao kutoka nchi saba walikutana nchini huko kwa lengo la kuangalia mbinu za kuboresha masuala ya soka ndani ya ukanda huo wa Afrika Mashariki na Kati.
Mara baada ya kumaliza kikao chao Magogo aliwatembeza wageni wake kwenye jengo hilo la ghorofa moja na kuonekana kushangazwa na miradi iliyomo ndani yake.
Moja kati ya kitu kilichowapa 'Suprise' ni kuona Shirikisho hilo likimiliki kituo cha Redio cha michezo 102.1 FUFA Fm ambacho kinadaiwa ni moja kati ya matumizi mazuri ya fedha za mgao walizopata kutoka CAF.
Fedha hizo ambazo zinadaiwa ni kiasi cha Dola za Kimarekani Laki mbili ($200,000) pia zilidaiwa kutumwa kwa mashirikisho mengine ikiwemo TFF kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi na miundo mbinu mengine.
Kituo hicho cha redio kimeleta tija sana kwa FUFA kutokana na kusambaza taarifa zao kwa wakati zinazohusiana na michezo sambamba na kutoa ajira kwa baadhi ya waandishi wa habari.
Aidha katika ofisi hizo kuna maduka kadhaa ambayo miongoni mwao yanatumika kwa ajili ya kuuzia fulana ama sare za timu ya Taifa ya nchi hiyo.
Imani yangu ni kwamba Marais hao walijifunza mengi kutoka kwa Shirikisho hilo na huenda tukaona maboresho kwenye ofisi zao.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.