Habari za Punde

Maadhimisho ya Siki ya Urithi wa Dunia Uhifadhi wa Miji Mikongwe Duniani Zanzibar.

Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar  Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Uhifadhi ya Mji Mkongwe Zanzibar Mohammed Baloo alipowasili katika viwanja vya Ngome Kongwe kupokea maandamano na kuzungumza wakati wa sherehe hizo za maadhimisho ya Siku ya Urithi wa Dunia Uhifadhi wa Mji ya Historia Duniani. yalioadhimishwa katika viwanja vya Ngome Kongwe Mji Mkongwe wa Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Balozi Ali Karume, alipowasili katika viwanja vya Ngome Kongwe Zanzibar katikati Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe Ayoub Mohammed Mohmoud.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa na Viongozi wa Serikali na Jumuiya wakisubiri kupokea maandamano ya kuadhimisha Siku ya Urithi wa Dunia ilioadhimishwa katika viwanja vya Ngome Kongwe Zanzibar. 
Maandamani ya Wananchi wanaokaa katika maeneo ya Uhifadhi ya Mji Mkongwe Zanzibar wakiwa katika maandamano hayo kuadhimisha Siku ya Urithi wa Dunia wa Uhifadhi miji mikongwe wakipita mbele ya mgeni rasmin Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, katika viwanja vya ngome kongwe Zanzibar maandamano hayo yameazia katika viwanja vya malindi darajani na kumalizikia Ngome Kongwe.  
Wananchi wa mji mkongwe wa Zanzibar wakishiriki katika maandamano hayo ya kuadhimisha Siku ya Urithi wa Dunia wa Uhifadhi wa Miji Mikongwe Duniani.

Wananchi wa Shehia mbalimbali za Mji Mkongwe wakishiriki katika maandamano hayo ya kuadhimisha Siku ya Urithi wa Dunia.
Mkurugenzi wa Uhifadhi wa Mji Mkongwe wa Zanzibar Issa Makarani akitowa maelezo ya Uhifadhi wea Mji Mkongwe wa Zanzibar wakati wa sherehe hizo za Siku ya Urithi wa Dunia, zilizofanyika katika viwanja vya Ngome Kongwe Zanzibar.  
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozo Seif Ali Iddi akiwa na viongozi wa meza kuu wakimsikiliza Mkurugenzi wa Hifadhi ya Mji Mkongwe wa Zanzibar akitowa maelezo wa uhifadhi wa Mjini Mkongwe Zanzibar wakati wa hafla hiyo ya Siku ya Urithi wa Dunia katika viwanja vya Ngome Kongwe Zanzibar.
Muakilishi wa Jumiya ya ACRA Laura Macini akitowa salamu za Acra wakati wa hafla hiyo ya uhifadhi wa Mji Mkongwe wa Zanzibar katika viwanja vya Ngome Kongwe Zanzibar. 
Wanafunzi wa Skuli ya Darajani Msingi wakisoma maulid ya home wakati wa hafla hiyo ya Siku ya Urithi wa Dunia uhifadhi Mji Mkongwe Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwasalimia na kuwapongeza Wanafunzi wa Skuli ya Msingi ya Darajani Zanzibar kwa kuonesha umahiri wao katika kusoma maulid ya home, wakati wa hafla hiyo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwasalimia na kuwapongeza Wanafunzi wa Skuli ya Msingi ya Darajani Zanzibar kwa kuonesha mavazi ya utamaduni mbalimbali wakati wa hafla hiyo.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.