Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Zuberi Ali Maulid na Viongozi wa Timu ya Zaee Sport Club ya Arusha wakifuatilia mchezo wao wa kirafiki kuadhimisha Tamasha la Pasaka katika viwanja vya Amaan Zanzibar Timu ya Wazee ya Arusha imeshinda kwa mabao 2--1 Katika Tamasha hilo lilijumuisha michezo mbalimbali ya kufuta kamba resi za magunia na kufukuza kuku.
Viongozi na Wapenzi wa Timu ya Wazee Sport Club ya Arusha wakifuatilia mchezo wao na marafiki zao Timu ya Baraza la Wawakilishi wakati wa kuadhimisha Tamasha la Michezo ya Pasaka kati ya Timu hizo mbili mchezo uliofanyika katika viwanja vya Amaan Zanzibar.
Viongozi na Wapenzi wa Timu ya Wazee Sport Club ya Arusha wakifuatilia mchezo wao wa kirafiki kuadhimisha Tamasha la Pasaka lililofanyika katika viwanja vya Amaan Zanzibar.

Wafanyakazi wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakifuatilia Tamasha hilo katika Viwanja vya Amaan Zanzibar.
Viongozi wa Timu ya Baraza la Wawakilishi wakifuatilia mchezio huo wa Tamasha la Pasaka na Timu ya Wazee Sport Club ya Arusha mchezo uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar Timu ya Wazee imeshinda 2--1
Timu ya Baraza la Wawakilishi ikitowa uwanja baada ya kipindi cha kwanza kumalizika wakiwa nyuma kwa bao 2--0.
Kocha Mkuu wa Timu ya Wazee Sport Club ya Arusha akitowa maelekezo kwa wachezaji wake wakati wa mapumziko ya kipindi cha kwanza wakiwa mbele kwa bao 2--0.
Kocha Mkuu wa Timu ya Baraza la Wawakilishi Juma Sumbu akitowa maelekezo kwa timu yake ikiwa nyuma kwa mabao 2--0.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Zuberi Ali Maulid akiongozana na Kiongozi wa Timu ya Baraza la Wawakilishi Dau akielekea kukagua timu hizo kipindi cha Pili kutokana na mvua iliokuwa ikinyesha wakati wa mchezo huo.
No comments:
Post a Comment