MITI mbali mbali ikiwa imeanguka katika moja ya
sehemu ya Barabara ya Chake-Mkoani, kufuatia mvua kubwa iliyonyesha Kisiwani
Pemba.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
MAGUNIA 518 ya Karafuu Kavu zikiwa hazikuharibika
katika ghala la kuhifadhia karafuu la Shirika la ZSTC Mkoani, baada ya ghala
hilo kuanguka sehemu ya Ukuta na gunia tisa kufukiwa na dongo zikiwa na karafuu
kavu.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
SEHEMU ya Ghala la Kuhifadhia karafuu la ZSTC
Mkoani, likiwa limebomoka baada ya kuangukiwa na mti uliokuwa katika mlima na
kupelekea Gunia Tisa za Karafuu Kavu zenye thamani ya Zaidi ya Milioni 5
kufukiwa na dongo kutokana na mvua kubwa iliyonyesha Kisiwani Pemba.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
WATOTO wadogo wakisafisha kwa kutoa dongo nje katika
Msikiti wa Mbuyuni Wilaya ya Mkoani, baada ya sehemu kubwa ya msiki huo
kuangukiwa na Udongo ulioporomoka na kuharibu Msikiti, kama unavyoonekana katika
Picha.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
WATOTO wadogo wakisafisha kwa kutoa dongo nje katika
Msikiti wa Mbuyuni Wilaya ya Mkoani, baada ya sehemu kubwa ya msiki huo
kuangukiwa na Udogo ulioporomoka na kuharibu Msikiti, kama unavyoonekana katika
Picha.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
WANANCHI wa Mbuyuni Wilaya ya Mkoani, wakitoa msaada
kwa kuondosha Udongo, ili kutoa Vitu vilivyofukiwa na Fusi baada ya Nyumba ya Fadhil
Amour Mohamed kuangukiwa na Udongo na kutokupata hata kitu Kimoja.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
MOJA ya nyumba wanazoishi wananchi katika shehia ya
Mbuyuni Wilaya ya Mkoani, ikiwa imeelemewa na Udongo uliokatika katika mlima,
uliopelekea nyumba hiyo kuvunjika sehemu ya Ukuta huo, kufuatia mvua
zinazoendelea kunyesha Kisiwani Pemba.(PICHA
NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
KIJIKO cha Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na
Usafirishaji Pemba, kikiondosha dongo lililoporomoka katika milima na kuingia
barabarani, kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha Kisiwani Pemba.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
ZAIDI ya Mita 150 katika barabara ya Mgagadu Kiwani
eneo la Darajani, likiwa limeharibiwa Vibaya na Mvua zinazoendelea Kunyesha
Kisiwani Pemba.(PICHA NA ABDI SULEIMAN,
PEMBA)
VIONGOZI
mbali mbali wa Serikali wakiongoza na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba,
Mhe:Mwanajuma Majid Abdalla, wakikagua sehemu ya barabara ya Mgagadu Kiwani
Ilivyoharibika kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha Kisiwani Pemba.(PICHA NA ABDI SULEIMAN,
MATUMAINI ya wananchi kupata kilimo chao cha mpunga
walichokilima kwa muda mrefu yameanza kupotea, kufuatia mashamba ya kilimo
hicho kujaa maji mengi kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha Kisiwani Pemba.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
MIONGONI mwa Nymba 58 za wananchi wa shehia ya
Mwambe Wilaya ya Mkoani, zilizoharibiwa na mvua zinazoendelea kunyesha kisiwani
Pemba.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
MVUA
zinazoendelea kunyesha Kisiwani Pemba, zimeanza kuleta madhara kwa wananchi
wanaoishi, Pichani baadhi ya vitu vya mmoja wa wananchi wa Shehia ya Wambaa
vikiwa nje baada ya nyumba yake kujaa maji.(PICHA
NA ABDI SULEIMAN, PEMBA
VIONGOZI mbali mbali wa Serikali wakiongoza na Mkuu
wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mhe;Mwanajuma Majid Abdalla, akiwangalia daraja la
Pujini lililowatenganisha wananchi wa Pujini na Chake Chake baada ya sehemu ya
barabara hiyo kukatika, kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha Kisiwani
Pemba.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
WANANCHI wa Kipapo Mgelema wako hatarini kukosa
barabara ya kupita baada ya mvua kubwa iliyonyesha Kisiwani Pemba, kuharibu
barabara yao.(PICHA NA ABDI SULEIMAN,
PEMBA)
Mola awape subra katk kipindi hiki kigumu
ReplyDelete