Habari za Punde

Serikali kuanzisha mfuko maalum wa kinga ya msingi Maskulini kujikinga dhidi ya uhalifu na Dawa za kulevya

 Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Ahmad Kassim  Haji kati kati aliyevaa Suti nyeusi akikiongoza Kikao cha maandilizi ya kuanzishwa mafunzo maalum ya kinga ya msingi Maskulini kwa lengo la  kutoa elimu itakayowasaidia wanafunzi kujikinga dhidi ya uhalifu na Dawa za kulevya.

 Mshauri wa Kanda ya Afrika Mashariki wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia mapambano dhidi ya uhalifu na Dawa za kulevya      { UNODC } Bibi Sylvie Bertrandwa Pili kutoka kushoto akifafanua jambo juu ya mpango huo utakaosimamiwa na UNODC.

Picha na – OMPR – ZNZ.

Na Othman Khamis, OMPR

Uongozi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia mapambano dhidi ya uhalifu na Dawa za kulevya { UNODC } umeamua kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika  kuanzisha mafunzo maalum ya kinga ya msingi Maskulini kwa lengo la  kutoa elimu itakayowasaidia kujikinga dhidi ya uhalifu na Dawa za kulevya.

Uongozi huo umekutana na  Watendaji wa Tume ya Udhubiti wa Dawa za Kulevya pamoja na wale wanaosimamia udhibiti wa uhalifu Chini ya Mwenyekiti wake Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Ahmad 
Kassim Haji  Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.

Mshauri wa Kanda ya Afrika Mashariki wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia mapambano dhidi ya uhalifu na Dawa za kulevya { UNODC } Bibi Sylvie Bertrand alisema mpango huo wa Mafunzo utashirikisha Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar.

Bibi Sylvie alisema katika kuupa nguvu zaidi mpango huo ili ufanikiwe vyema Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto pia itakuwa mshirika katika mpango huo utaoratibiwa na Tume ya Kudhibiti Dawa za Kulevya Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.