Habari za Punde

ZIRPP MONTHLY LECTURE: "Miaka 53 ya Muungano na Safari ya Kutafsiri Mfumo wa Muungano"

Dear Members and Friends,
I have the pleasure to kindly inform you that there will be another ZIRPP Monthly Lecture.
Chairperson: Mr. Muhammad Yussuf

Speaker: Mr. Othman Masoud Othman
Subject: "Miaka 53 ya Muungano na Safari ya Kutafsiri Mfumo wa Muungano"
Date & Time: Saturday 29th April 2017; at 4:00 pm.
Venue: ZIRPP Office,Third Floor, behind Majestic Cinema (above ZANLINK
ABSTRACT: Katika shamra-shamra za kusherehekea miaka 53 ya Muungano wa Tanzania, ni vyema kujikumbusha kuwa mambo mengi ya Muungano yamefanyika na kubadilika kwa kutegemea miongo ya kisiasa. Jambo moja ambalo limedumu katika miongo yote ya majira ya Muungano ni suala la kupata tafsiri sahihi ya Muungano kikatiba, kisheria, kisiasa na kiutendaji. Safari hii ya kutafuta tafsiri imewajumuisha wanataaluma, wanasiasa na hata watu wa kawaida. Kukosekana kwa ramani ya safari yenyewe, safari ya kutafuta tafsiri sahihi ya Muungano imekuwa ngumu. Wapo waliopata maafa katika safari hii na kuna wakati mwengine tafsiri imeleta fadhaa kubwa nchini. Naiwe iwavyo, safari ya kutafuta tafsiri sahihi ya Muungano bado inaendelea.
Kwa mfano, kukubaliwa kwa Zanzibar hivi karibuni kuwa mwanachama wa 54 wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Afrika ni moja kati ya matukio muhimu katika jitihada za kuutafsiri Muungano wa Tanzania. Wapo wanaojiuliza, jee tukio hili ni mawio au machweo katika safari ndefu ya kupata tafsiri halisi na sahihi ya Muungano?
Kutokana na historia na umuhimu wa suala hili kwa mustakbali mwema wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ZIRPP imemualika aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Zanzibar na Mwanasheria maarufu aliyebobea katika masuala ya katiba na sheria, Mheshimiwa Othman Masoud Othman, kuja kulijadili suala hili kwa kina ikiwa ni sehemu moja katika pirika-pirika za kusherehekea kutimia miaka 53 ya Muungano wa Tanzania.
Tea, Coffee and Snacks will be served freely.
Please forward this message to anybody who may be interested. Those who would like to attend should send their email addresses and telephone numbers to: zirpp@googlegroups.com.
Please confirm your participation. You may bring one or two friends with you.
All are welcome.
Muhammad Yussuf
Executive Director
Zanzibar Institute for Research and Public Policy
P.O. Box 4523, Zanzibar, Tanzania;
Tel: +255 242 223-8474;
Fax: +255 242 223-8475;
Cellular: 0777 707820;
Website: www.zirpp.info

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.