Habari za Punde

Bohari kuu wamuaga aliekuwa mkuu wa kitengo cha kusambaza dawa Zanzibar

 Mkuu wa Utawala na Uendeshaji wa Bohari Kuu ya dawa Zanzibar akitoa maeleza ya utendaji kazi wa aliekuwa mfanyakazi wake Abdalla Suleiman aliemaliza muda wa utumishi Serikalini katika sherehe zilizofanyika  Ofisini kwao Maruhubi nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
 Aliekuwa mkuu wa Kitengo cha kusambaza dawa Zanzibar Abdalla Suleiman akiwa na mke wake Dkt. Aza Said wakimsikiliza Mkuu wa Utawala na Uendeshaji Bohari Kuu ya dawa katika sherehe za kumuaga zilizofanyika Maruhubi.

 Mkurugenzi Utumishi na Uendesha Wizara ya Afya Zanzibar Ramadhan Khamis Juma, aliekuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo, akimpongeza  mstaafu Abdalla Suleiman kwa kukamilisha majukumu yake vizuri Serikalini.
 Aliekuwa Mkuu wa Kitengo cha kusambaza dawa Zanzibar Abdalla Suleiman akiwapa mkono wa kwaheri wafanyakazi wenzake katika sherehe za kumuaga, wa kwanza (kushoto) Mkurugenzi wa Bohari Kuu ya dawa Zahran Ali Hamad na (kati) Mkurugenzi Utumishi na Uendeshaji Wizara ya Afya Ramadhan Khamis Juma.
Picha ya pamoja ya mstaafu wa Bohari Kuu Abdalla Suleiman akiwa na mke wake Dkt. Aza Said (kulia) waliokaa na baadhi ya  wafanyakazi wa Bohari kuu ya dawa na Ofisi ya Mfamasia Mkuu katika sherehe za kumuaga zilizofanyika Bohari Kuu ya dawa Maruhubi.

Picha na Makame Mshenga.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.