Habari za Punde

Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Afanya Kikao na Wafanyakazi wa Ofisi Hiyo na Kuwataka Kufanya Kazi Kwa Bidii.

Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akizungumza wakati wa kikao cha wafanyakazi wa ofisi hiyo kilichofanyika leo katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam. Katika kikao hicho, Dkt.Chuwa amewataka wafanyakazi hao kufanya kazi kwa bidii na weledi ili kuboresha zaidi upatikanaji wa takwimu rasmi nchini
Kaimu Mkurugenzi wa Utawala, Fedha na Masoko Bi. Lilian Karumuna wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu akifafanua jambo wakati wa kikao cha wafanyakazi wa ofisi hiyo kilichofanyika leo katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam
Katibu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania tawi la Ofisi ya Taifa ya Takwimu (TUGHE) Bi. Raya Mikidadi akifafanua jambo wakati wa kikao cha wafanyakazi wa ofisi hiyo kilichofanyika leo katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam
Baadhi ya wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mkuu Dkt. Albina Chuwa (hayupo pichani) wakati wa kikao cha wafanyakazi wa ofisi hiyo kilichofanyika leo katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam
Baadhi ya wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mkuu Dkt. Albina Chuwa (hayupo pichani) wakati wa kikao cha wafanyakazi wa ofisi hiyo kilichofanyika leo katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam. (Picha na Veronica Kazimoto)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.