Habari za Punde

UVCCM yashitukia mchezo mchafu kisiasa

Na Mwandishi wetu, Rukwa

Umoja wa Vijana wa CCM umewaonya watendaji wake kujiepusha na uvunjaji wa kanuni na maadili ya jumuiya  hiyo ikiwemo kuendesha mijadala inayozmgumzia masuala ambayo yaliopitishwa kwa mujibu wa vikao,  kikanuni na katiba ya CCM.  

Pia umoja huo umelaani na kusema kitendo chochote  cha utovu wa nidhamu na ukiukaji maadili kitakachothibitika kufanywa na mtendaji husika katika ngazi ya jumuiya hatua za kimaadili na kikanuni zitafuata haraka sana.

Msimamo huo umetolewa  na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka alipokuwa akizungumza kwa nyakati tofauti na watendaji wa jumuiya hiyo ngazi za matawi, kata na wilaya na mkoa katika mkoa wa Katavi na Rukwa.  

Shaka alisema jumuiya ina taarifa za kutosha kwamba kuna baadhi ya watendaji wanatumiwa na maadui ili kutaka kudhoofsha juhudi na mikakati ya umoja huo kwa njia za mitandao ya kijamii na magazeti. 

Alisema UVCCM itatumia njia na vyanzo vyake muhimu kupata ushahidi kamili dhidi ya wanaoshiriki  uhalifu huo na kuchukua hatua stahiki za kinidhamu na kanuni  dhidi ya watendaji hao ikiwemo 
kutaja majina yao na wanaoshirikiana nao .

"Zipo juhudi na mikakati batili ambayo naamini haitafua dafu ya kutaka
 kuichafua jumuiya yetu kwa maneno ya uzushi na upotoshaji, inashangaza  kusikia baadhi ya watendaji wetu nao wanashiriki kucheza ngoma hiyo ya wachawi wa CCM na jumuiya zake tunajuwa na tunatafahamu yako makoloni ya watu bado yamo ndani tumeshakula kiapo tutambana nao na tunawahakikishia CCM iatabaki salama hawatafanikiwa nia zao ovu "Alisema Shaka akionekana kukerwa. 

Aliwaeleza watendaji hao kwamba kila uamuzi unaofanyika ndani ya chama na jumuiya zake ni maamuzi yanayopitishwa kikanuni na kikatiba bila kukiukwa utaratibu au miongozo husika.  

Aidha shaka aliwakanya watendaji na wana jumuiya ambao wanadhani hoja zao zinaweza kuwa na mashiko au nguvu kuliko matakwa na mashari ya msingi  yatokanayo na kanuni na katiba ya CCM .

"Nmekuwa nikipigiwa simu nyingi na baadhi ya waandishi wakidai kuna watendaji wa uvccm wanapigana uteuzi wa Nafasi fulani wengine wakienda kudai madai kwenye vyombo vya habari hivi 
unapingaje maamuzi ya kikanuni na kikatiba, anayepinga maamuzi hayo anatumwa kwa nguvu za kishetani na unakwendaje kudai madai ya uhamisho kupitia vyombo vya habari sio maadili ya uongozi wa chama chetu chama hiki kinautaratibu mzuri sana wa kushuhulikia mambo yake ya ndani kuanzia kata shina hadi taifa:Akieleza .

Kaimu huyo Katibu Mkuu alisema wapo watu ambao awali walidhani  jumuiya ya umoja wa vijana wa CCM  isingekuja juu na kusimamia misingi yake hivyo wanapona kuna ishara njema za mafanikio wameamua kuanza kutunga na kuzusha mambo ya yasiyo ya msingi.  

"Wana jumuiya wahoji masuala ya msingi yanayohusu uhai na maendeleo ya uvccm ni haki yao lakini watumie  vikao halali vya kikanuni na kikatiba kuelezea hoja zao na madai yao ikiwa ya ufisadi au wizi huku wakionyesha ushahidi, kulalamika mitandaoni na magazetini hakuleti ufumbuzi wala hawakisaidi chama na jumuiya na sio utamaduni wa Chama Cha Mapinduzi chama chetu ni kikubwa kina maadili na miongozo yake hatuwezi kuvumilia vitendo vya utovu wa nidhamu na ukosefu wa maadili ya uongozi" Alisistiza kaimu huyo Katibu Mkuu. 


Shaka amekamilisha ziara ya kuimarisha uhai wa Chama na jumuiya zake katika mikoa Katavi na Rukwa na kesho (Leo) anatarajiwa kuanza ziara ya kikazi katika mikoa ya Pwani na Dar es Saalam kutembelea wilaya zote za mikoa hiyo.
 


End

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.