Habari za Punde

Wazanzibari tumuombee dua Mohammed Issa ( Banka) tunzo ya mchezaji chipukizi Ligi Kuu T/Bara 2016/17

WAZANZIBAR TUMUOMBEE DUA MOHAMMED BANKA KESHO KUSHINDA TUNZO YA MCHEZAJI CHIPUKIZI  LIGI KUU TANZANIA BARA 2016/17

Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Kiungo wa Timu ya Mtibwa Sugar Mohammed Issa  “Banka” wengine wanamfamu kwa jina la Mudy Gold ambae ni Mzanzibar amefanikiwa kuingia kwenye orodha ya majina matatu ya wachezaji wanaogombea tunzo ya mchezaji bora anayechipukia kwenye ligi kuu soka Tanzani bara ambayo imehitimishwa Jumamosi iliyopita.

Banka ameonesha kiwango cha hali ya juu akicheza kwa mara ya kwanza ligi kuu soka Tanzani bara msimu huu ambapo alitokea klabu ya Chuoni Visiwani Zanzibar ambapo amechaguliwa kuwemo kwenye kinyanganyiro cha tunzo hiyo.

Sherehe za Tunzo hizo zitafanyika  kesho Jumatano Mei 24 mwaka huu kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Wachezaji wengine ambao wanawania tunzo hiyo ni Mbaraka ABEID wa Kagera Sugar na Shaaban IDD wa Azam FC.

Mtandao huu umemtafuta kiungo huyo ambae kwasasa yupo hapa kwao Visiwani Zanzibar na kusema kuwa amefurahishwa mno kuwemo kwenye orodha ya wachezaji wanaowania tunzo hiyo ikiwa yeye ndio mara yake ya kwanza kucheza ligi hiyo.

“Mimi namshukuru Mwenyezi Mungu kuwemo katika orodha ya majina matatu tunaowania tunzo ya mchezaji anaechipukia, namuomba Mungu anijaalie nishinde na pia ni faraja kwangu kwani ndo msimu wangu wa kwanza kucheza ligi ya bara kisha kuchaguliwa, nawaomba Wazanzibar waniombee dua nishinde na tuzidi kuonesha viwango kwani Zanzibar tuna vipaji vingi sana”. Alisema Banka.

Mbali ya tunzo hiyo ya mchezaji anaechipukia pia kuna tunzo tofauti zinazowaniwa zikiwemo:-

Tunzo ya Heshima (ambayo itatolewa kwa mwanasoka nguli wa zamani mwenye historia nzuri kwa soka la Tanzania).

Nyingine  ni: Tuzo ya Kikosi Bora cha Msimu (Itatolewa kwa wachezaji Bora 11 wa Ligi Kuu (VPL XI 2016/2017) walioteuliwa kutokana na ufanisi wao katika ligi hiyo msimu huu.

Pia imeongezwa Tuzo ya Mchezaji Bora mwenye chini ya umri wa miaka 20 (Hii itatolewa kwa wachezaji waliofanya vizuri katika ligi ya vijana ya timu za Ligi Kuu ya Vodacom.

Tuzo hiyo ya Mchezaji Bora wa Ligi ya Vijana itajulikana kama Tuzo ya Ismail Khalfan ikiwa ni heshima ya kumbukumbu ya mchezaji Ismail Khalfan wa Mbao FC aliyefia uwanjani katika mashindano hayo yaliyofanyika mkoani Kagera.

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limefikiria kutoa tuzo hiyo kama njia mojawapo ya kuonesha kuthamini kipaji cha mchezaji huyi wakati wa uhai wake.

Kutokana na mabadiliko hayo tuzo zitakazotolewa katika sherehe hizo pamoja na Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya VPL ambayo ndiyo tuzo kuu, pia ni Bingwa wa Ligi Kuu, Mshindi wa Pili, Mshindi wa Tatu, Mshindi wa Nne na  Mfungaji Bora.

Nyingine ni Mchezaji Bora wa Ligi Kuu, Golikipa Bora, Kocha Bora, Mwamuzi Bora, Mchezaji Bora wa Heshima, Mchezaji Bia anayechipukia, Goli Bora la Msimu, Mchezaji Bora wa Kigeni, Mchezaji Bora wa Chini ya Umri wa Miaka 20 na Timu Yenye Nidhamu.

Tuzo za Bingwa, mshindi wa pili, wa tatu na wa nne na Mfungaji Bora hizi zipo kulingana na msimamo wa ligi ulivyo.

Hata hivyo Mfungaji Bora safari hii kuna wachezaji wawili wamefungana, Abdulrahman Mussa wa Ruvu Shooting na Simon Msuva wa Yanga wameibuka wafungaji bora kwenye Ligi Kuu Soka ya Tanzania Bara msimu wa 2016/2017 iliyomalizika Mei 20 mwaka huu.

Kutokana na wachezaji hao kuibuka vinara kwa ufungaji ambapo kila mmoja amefunga mabao 14, watagawana zawadi ya mfungaji bora ambayo ni sh. 5,800,000.


Wafuatao wameteuliwa kuwania tuzo hizo kutokana na vigezo mbalimbali:

Mchezaji Bora wa Ligi Kuu
Aishi MANULA - Azam
Simon MSUVA - Yanga
Shiza KICHUYA - Simba
Haruna NIYONZIMA - Yanga
Mohammed HUSSEIN – Simba
(Majina ya wanaowania tuzo hiyo yalitolewa Jumatano iliyopita na upigaji kura unaendelea ukiwahusisha Makocha wa timu za Ligi Kuu na Makocha Wasaidizi,Wahariri wa habari za michezo na Manahodha wa timu za Ligi Kuu, ambapo mwisho wa kufanya hivyo ni leo Jumanne Mei 23 mwaka huu).

KIPA BORA
Aishi MANULA - Azam
Owen CHAIMA - Mbeya City
Juma KASEJA - Kagera Sugar

KOCHA BORA
Joseph OMOG - Simba
Mecky MEXIME - Kagera Sugar
Ettiene NDAYIRAGIJE - Mbao

MWAMUZI BORA
Shomari LAWI – Kigoma
Elly SASII – Dar es Salaam
Hance MABENA - Tanga

MCHEZAJI BORA WA KIGENI
Haruna NIYONZIMA - Yanga
Method MWANJALE - Simba
Yusuph NDIKUMANA - Mbao

MCHEZAJI BORA ANAYECHIPUKIA
Mbaraka ABEID - Kagera Sugar
Shaaban IDD - Azam
Mohammed ISSA (Banka) - Mtibwa

TUZO YA ISMAIL KHALFAN – (U-20)
Shaaban IDD - Azam
Abdalah MASOUD - Azam
Mosses KITAMBI - Simba

TUZO YA HESHIMA
(Atatangazwa aliyeteuliwa siku hiyohiyo ya sherehe za tunzo yani kesho).

GOLI BORA LA MSIMU
(Tayari yamepatikana mabao bora 10 ambayo yataoneshwa siku hiyo ukumbini ikiwemo lile bora la msimu mzima).

TIMU YENYE NIDHAMU
(Mshindi atatangazwa ukumbini siku hiyo kulingana na vigezo vilivyopo).

WACHEZAJI 11 BORA WA MSIMU – VPL XI 2016/17
(Watatangazwa ukumbini siku hiyo ya sherehe, yani kesho).


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.