Habari za Punde

TFF lapeleka maombi rasmi FIFA kuiombea Zanzibar uanachama wa Shirikisho la Soka Duniani {FIFA}. Afisa Muandamizi anayeshughulikia ruzuku wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania {TFF} Derek Murusuri aliyevaa Suti rangi ya Wardi akiwasilisha Salamu za Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania Jamal Malinzi  kwa Makamu wa Pili wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi  za kuiombea Zanzibar uanachama wa Shirikisho la Soka Duniani {FIFA}.

  Derek Murusuri akimueleza Balozi Seif Mikakati ya TFF ya kuwa na Timu bora ya Soka itakayoiwezesha Tanzania kishiriki mashindano ya Kombe la Dunia ifikapo mwaka 2026.
Makamu wa Pili wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiishukuru  TFF kwa hatua iliyifikia ya kuiombea Zanzibar uanachama katika Shirikisho la Soka Duniani FIFA.

Picha na  - OMPR – ZNZ.


 Na Othman Khamsi Ame, OMPR

Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini  Tanzania {TFF }limepeleka maombi kwenye Shirikisho la Soka Duniani { FIFA } kuiomea Zanzibar kuwa Mwanachama wa Shorikisho hilo.

Kauli hiyo imetolewa na Afisa Muandamizi anayeshughulikia ruzuku wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania {TFF} Derek Murusuri wakati akiwasilisha salamu za Rais wa Shirikisho hilo Jamal Malinzi kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Baraza la Wawakilishi Mbweni.

Derek Murusuri alisema Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania limeshaiandikia Barua rasmi FIFA kuhusu suala hilo lilalosubiriwa na wapenda soka wa Visiwa vya Zanzibar kuwa na uweo wa kushiriki moja kwa moja michezo ya Kimataifa inayoandaliwa na Shirikisho hilo la Dunia.

Alisema mipango inaandaliwa na Uongozi wa juu wa TFF katika kuhakikisha inaipatia nakala Zanzibar  kuthibitisha hatua zilizokwishachukuliwa na Uongozi huo wa juu wa Soka Tanzania.

Afisa Muandamizi huyo anayeshughulikia ruzuku wa TFF alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba TFF hivi sasa  inaendelea na mikakati ya kukusanya Vijana wenye vipaji kwa lengo la kuwandaa kupitia mashindano mbali mbali ya Kitaifa na Kikanda kwa kuwaona ili kupata Timu imara itakayokuwa na uwezo wa kushiriki Kombe la Dunia mwaka 2026.


Aliipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushirikiana na Taasisi zake zinazosimamia michezo pamoja na washirika wa Sekta hiyo kwa  juhudi ilizochukuwa za kuisaidia Timu ya Taifa ya Viwanja wenye umri wa chini ya miaka 17 ya Serengeti Boys.

Alisema Timu hiyo kwa kiasi kikubwa imeweza kuipa heshima kubwa Tanzania kwa kiwango ilichofikia katika mashindano ya hivi karibuni ya kuwania Kombe la Dunia linalotarajiwa kufanyika India kwa  kutolewa na Timu ya Soka ya Niger katika hatua ya Robo Fainali.

Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliupongeza Uongozi mzima wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania kwa hatua uliofikia wa kuisimamia Zanzibar katika  maombi hayo.

Balozi Seif alisema Zanzibar imekuwa katika harakati za kutafuta fursa ya kuwa mwanachama wa Shirikisho la Mpira wa Soka Duniani FIFA kwa kipindi kirefu sasa licha ya vikwazo na changamoto nyingi zilizojitokeza na kukwaza ucheleweshaji huo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.