Habari za Punde

TIRA yaja na mwarubaini kukomesha bima feki

NA HAJI NASSOR, PEMBA

MAMLAKA ya Usimamizi wa Bima Tanzania ‘TIRA’ imesema sasa imefika mwisho wa mawakala na makampuniza na uuzaji wa bima za vyombo vya moto zisizotambulika ‘feck’, bada ya Mamlaka hiyo, kuwa na njia za kielektroniki za uhakikiwa bima hizo.

Mmlaka hiyo imesema, kwa muda mrefu wamiliki wa vyombo vya moto, wamekuwa wakiuziwa bima zisizostahiki bila ya wao kujua, ingawa kwa sasa kwa wauzaji hao, mwisho wao umefika.
Akizungumza kwenye mafunzo ya siku moja, yaliowahusishwa askari wa kikosi  cha usalama barabarani na kufanyika skuli ya sekondari Madungu Chakechake, Mkurugenzi wa Masoko na utafiti wa Mamlaka hiyo Adelaida Muganyizi alisema sasa bima zote zitahakikiwa kwa njia ya kielektroniki.

Mkurugenzi huyo alieleza kuwa, kwa vile kisheria kila kampuni au wakala wa kuuza bima anatakiwa awe amesjaliwa na Mamlaka ya usimamizi wa bima Tanzania ‘TIRA’ itakuwa ni rahisi kuwashika wale mawakala wanaofanyakazi zao kimagumashi.


Alieleza kuwa, kupitia mfumo wa kisasa wa kuandika neno stika ikifuatiwa na namba ya bima na kuituma kwenda namba 15200, kwa milikiwa gari au chombo cha moto atagundua uhalali wa wakala huyo.
“TIRA baada ya kukaa na wataalamu sasa imekuja na mfumo wa kidigitaji kwa anaenunua bima kabla ya kulipa, atafuata maelekezo hayo na kutuma kwenye namba husika, na hapo sasa atagundua kuwa muuza bima huyo anatambuliwa na ‘TIRA’ au ni wa mitaani”,alieleza.
Kwa upande wake Menaja wa ‘TEHAMA’ wa Mamlaka hiyo Aron Malaki alisema, kazi iliopo mbele yao kwa sasa, ni kutoa elimu kwa wamiliki wa vyombo vya moto na wananchi wengine, juu ya kufuata mfumo huo wa kisasa.
“Faida yake hasa kwa abiria, iwapo gari haina bila halali ni vigumu unapopata ajali au kukugongwa kupata fidia kutokana na mauimivu ulioyapata kwa vile uhalali wa bima haupo”,alifafanua.


Mapema baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wa siku moja, wameiomba ‘TIRA’ kuhakikisha elimu hiyo wanaisambaaza kwa jamii nzima, ili kuhakikisha inawafikia.

Hata hivyo walisema kwa sasa wataondokana na ile njia ya zamani ya kukagua bima kwa kuangalia rangi na tarehe iliokatwa au kumalizika, na sasa kwa kutumia mfumo wa kisasa watafanyakazi wa uweledi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.