Habari za Punde

Wanamichezo wa Zanzibar wa UMISSETA Kuondoka Kesho Kuelekea Mkoani Mwanza Kushiriki Mashandano Hayo.

Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.
Zaidi ya wanamichezo 135 kutoka Unguja na Pemba wanatarajia kuondoka Visiwani Zanzibar kesho Jumamosi June 3, 2017 kuelekelea Butimba Mkoani Mwanza, kushiriki mashindano ya umoja wa Michezo na Sanaa skuli za sekondari Tanzania (UMISSETA).

Katika Mashindano hayo ambayo yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi lake Jumanne June 6, 2017 huko Butimba Chuo cha Ualimu Mkoani Mwanza, Zanzibar itakuwa na kanda mbili tofauti Unguja timu yao na Pemba timu yao, ambapo kanda ya Unguja itakuwa na timu za Soka, Wavu, Mikono, Riadha, Mpira wa Meza na Kikapu,wakati kanda ya Pemba itakuwa na timu za Riadha, Wavu, Kikapu na Soka.

Wanamichezo hao wataondoka  Zanzibar na boti ya jioni watalala Dar es Salaam na wanatarajia kuondoka Dar es Salaam kesho kutwa Jumapili Juni 4 kwa mabasi maalum ya kukodi kuelekea Mwanza, ambapo watawasili Jumatatu Juni 5 siku ambayo timu zote zinatakiwa ziwe zimewasili.
Attachments area

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.