Habari za Punde

ZFA kutoa taarifa ya jinsi ya kupatikana kwa timu 12 za Ligi Kuu Zanzibar Jumatatu



Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Chama cha Soka Visiwani Zanzibar (ZFA) kinatarajia kutoa taarifa Jumatatu ya June 19, 2017 ya kutaja tarehe ya kukutana timu 28 ambazo zitapendekeza mfumo gani utumike ili zipatikane timu 12 za ligi kuu soka ya Zanzibar za msimu ujao wa mwaka 2017-2018.

Tarehe hiyo ya kukutana vilabu hivyo 28 itatolewa siku hiyo ya Jumatatu majira ya saa 7:30 za mchana kwenye Afisi za ZFA zilizopo Amani Mjini Unguja.

Siku ya Alhamis Machi 16, 2017 itaendelea  kukumbukwa na Wazanzibar baada ya ZFA kuingizwa rasmi kuwa Mwanachama wa 55 wa Shirikisho la Soka Barani Afrika “CAF” kufuatia Kikao cha 39 cha Mkutano Mkuu wa Shirikisho hilo kilichofanyika Addis Ababa nchini Ethiopia.

Moja ya maagizo ya CAF ni kutaka msimu ujao wa mwaka 2017-2018 ligi kuu soka ya Zanzibar iwe na jumla ya timu 12 kwa Zanzibar nzima ambapo katika msimu huo wa mwaka 2016-2017 ulikuwa na jumla ya timu 36 kwa kila kanda ilikuwa ina timu 18, yani Kanda ya Unguja 18 na Kanda ya Pemba 18, huku zimeshashuka timu 12 kati ya hizo 36 kwa kila kanda zimeshuka timu sita (6).

Lakini Wadau wengi wa soka Visiwani Zanzibar wanahamu sana kujua mfumo gani utatumika kwaajili ya kupatikana timu 12 za ligi kuu soka ya Zanzibar kwa msimu ujao wa mwaka 2017-2018 ambapo Mkutano Mkuu wa dharura wa ZFA uliofanyika April 22 kwenye Ukumbi wa Uwanja wa Gombani Kisiwani Pemba ulipendekeza vilabu 28 vya ligi kuu ya Zanzibar vikutane kwa pamoja baada ya kumalizika 8 bora na kupanga ni mfumo gani utumike ili zipatikane timu 12 za msimu mpya.

Timu hizo 28 ni zile ambazo zimenusurika kushuka daraja katika mkumbo wa awali ambapo zimeshashuka timu 12 kwa kila kanda kushuka 6, yani Unguja 6 na Pemba 6 pamoja na zile nne za Daraja la Kwanza zilizofanikiwa kuja juu ambazo ni mbili Unguja na mbili Pemba ndizo zilizofanya kuwa na Jumla ya timu 28.

Viongozi wa timu hizo 28 za Unguja na Pemba watakutana kwa pamoja baada ya kutangazwa Jumatatu tarehe hiyo ya kukutana ndipo hapo patajulikana timu zipi zitacheza ligi kuu msimu ujao na mfumo gani utumike kupatikana kwa timu hizo 12.

Hivyo pengine mfumo utakaotumika huwenda timu ikawa imefanikiwa kuwa bingwa au Mshindi wa Pili wa Zanzibar (Wawakilishi wa Klabu Bingwa na Kombe la Shirikisho) lakini akashindwa kucheza ligi kuu ya Zanzibar kwa msimu ujao endapo akishindwa kuvuka katika  mfumo huo ambao utakaotumika.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.