Habari za Punde

Kocha Mkuu King Atangaza Kikosi cha Mwisho Cha Wachezaji 22 Kitakachowakilisha Michuano ya Rolling Stone Iliyopangwa Kuaza July 9 Mkoani Manyara.

Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.
Kocha Mkuu wa timu ya kombain ya Mjini Unguja Mohammed Seif “King”, jana usiku ametangaza kikosi cha mwisho cha wachezaji 22 kitakachoshiriki Mashindano ya Vijana ya Afrika Mashariki na Kati ya Rolling Ston yaliyopangwa kuanza July 9-19, 2017 huko Mbulu Mkoani Manyara.

Timu hiyo ambao ndio mabingwa watetezi wa mashindano hayo wanatarajia kuondoka Visiwani Zanzibar leo Alhamis usiku kwa boti inayoondoka usiku.

Wachezaji 22 waliyotangazwa na kocha King ni :-
WALINDA MLANGO
Aley Ali Suleiman “Manula” (Miembeni city), Ali Mabrouk “Al hapsy” Black Sailors na GeorgeMunish “Dida”.
WALINZI WA PEMBENI
Muharami Khamis “Terra” (Black Sailors), Abdul hamid Salum “Ramos” (KVZ) na Hassan Chalii (Kipanga).
WALINZI WA KATI
Ali Juma Maarifa “Mabata” (Taifa ya Jang’ombe) na Abubakar Ame “Luiz” (Membeni City).
VIUNGO WA KATI
Fahmi Salum (Mlandege), Ibrahim Chafu (Villa FC) Yakoub Amour (Jang’ombe Boys), Mohd Ridhaa (Villa United), Talib Hamad (Kipanga), Mohd Yahya “Banka” (Zimamoto),  Seif Said “Tiote” (KVZ) na Suleiman Ali “De Jong”.
VIUNGO WA PEMBENI
Abrahman Juma “Baby” (KMKM), Mohd Jailan (Chrisc), Mohd Haji “Box” (Jang’ombe Boys).
WASHAMBULIAJI
Ibrahim Abdallah “Imu Mkoko” (Miembeni City), Mohd Vuai “Prince” (Miembeni City) na Abdul hamid Juma “Samatta”.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.