Habari za Punde

Kocha wa Jamhuri akiri kwamba ligi bado ngumu

Kocha Mkuu wa timu ya Jamhuri, Abdulmutik Haji (Kiduu), ambae ana Leseni "A" alipokuwa akizungumza na waandishi baada ya moja ya mechi waliocheza uwanja wa Amaan

Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Kocha Mkuu wa timu ya Jamhuri, Abdul mutik Haji (Kiduu), amekiri ligi kuu ya Zanzibar hatua ya 8 bora ni ngumu na kwamba hadi sasa na hakuna timu ambayo imejihakikishia kutwaa ubingwa wa ligi hiyo inayofikia tamati Jumapili ya 20/8/2017.

Kiduu amesema licha ya timu yake kuongoza lakini bado ligi mbichi na timu zote 8 zina nafasi lakini atapigana kuhakikisha timu yake inaendelea kuongoza hadi mwisho wa ligi hiyo.

“Bado ligi ni ngumu mno, timu yoyote ina nafasi ya kutwaa ubingwa, mimi kubwa ntahakikisha naendelea kuongoza mpaka mwisho”. Alisema Kiduu.

Jamhuri ndie kinara wa ligi kuu soka ya Zanzibar hatua ya 8 bora akiwa na alama 12 akipata ushindi michezo yote 4 baada ya awali kuwafunga Mwenge mabao 3-2, kisha kuwachapa Okapi 3-0, wakaendelea kuwapiga Kizimbani 3-0 na juzi tu wakawamaliza Zimamoto kwa mabao 2-1.

Jamhuri watashuka tena Dimbani Ijumaa ya July 14, 2017 dhidi ya Taifa ya Jang’ombe saa 10 za jioni katika uwanja wa Amaan.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.