Habari za Punde

Kombaini ya mjini yafika salama Dar Alfajiri kuanza safari ya Manyara



Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Mabingwa watetezi wa Mashindano ya Vijana ya Afrika Mashariki na Kati ya Rolling Stone timu ya Kombain ya Mjini Unguja imewasili salama Jijini Dar es salam Alfajiri ya leo wakitokea Visiwani Zanzibar, na saa 12 za asubuhi wameanza safari kwa Basi ya kwenda Mbulu Mkoani Manyara katika Mashindano hayo yaliyopangwa kuanza July 9-19, 2017.

Jumla ya watu 30 wamo katika msafara huo wakiwemo wachezaji 22, makocha 2 pamoja na viongozi 6.

Wachezaji 22 waliyosafiri na timu hiyo ni :-
WALINDA MLANGO
 Aley Ali Suleiman “Manula” (Miembeni city), Ali Mabrouk “Al hapsy” Black Sailors na George Munish “Dida”.

WALINZI WA PEMBENI
Muharami Khamis “Terra” (Black Sailors), Abdul hamid Salum “Ramos” (KVZ) na Hassan Chalii (Kipanga).

WALINZI WA KATI
Ali Juma Maarifa “Mabata” (Taifa ya Jang’ombe) na Abubakar Ame “Luiz” (Membeni City).

VIUNGO WA KATI
Fahmi Salum (Mlandege), Ibrahim Chafu (Villa FC) Yakoub Amour (Jang’ombe Boys), Mohd Ridhaa (Villa United), Talib Hamad (Kipanga), Mohd Yahya “Banka” (Zimamoto),  Seif Said “Tiote” (KVZ) na Suleiman Ali “De Jong”.

VIUNGO WA PEMBENI
Abrahman Juma “Baby” (KMKM), Mohd Jailan (Chrisc), Mohd Haji “Box” (Jang’ombe Boys).

WASHAMBULIAJI
Ibrahim Abdallah “Imu Mkoko” (Miembeni City), Mohd Vuai “Prince” (Miembeni City) na Abdul hamid Juma “Samatta”.

Kocha mkuu wa timu hiyo ni Mohammed Seif “King” akisaidiwa na Ramadhan Abdulrahman “Madundo”.

Viongozi wengine walofatana na timu hiyo ni Hassan Haji Hamza “Chura” ambae ni mkuu wa msafara pamoja na Mwalimu Dau, Khamis Machano (Mwenyekiti wa Kamati ya Central Wilaya ya Mjini), Nassir Kheir (Mtunza vifaa), Said Salim “Hazard” (Muandishi wa Habari) na Nassir Salum “Msomali” (Muamuzi).

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.